Pata taarifa kuu

UN inahitaji msaada za Dolla Bilioni 2.8 kuwasaidia raia wa Palestine

Umoja wa Mataifa umetoa wito wa msaada wa Dolla za Marekani Bilioni 2.8 kuwasaidia zaidi ya raia Milioni tatu wa Palestine wanaohitaji msaada.

Raia wa Palestine waliopoteza makazi yao wakipokea msaada wa chakula kutoka kwa shirika la UN kuhusu misaada kwa Wapalestina (UNRWA). 28 janvier 2024.
Raia wa Palestine waliopoteza makazi yao wakipokea msaada wa chakula kutoka kwa shirika la UN kuhusu misaada kwa Wapalestina (UNRWA). 28 janvier 2024. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa UN hali ya Gaza kando na kuhitaji msaada wa chakula, raia pia wanahitaji kupewa maji safi pamoja na upatikanaji wa vituo vya kiafya.

Andrea De Domenico, Mkuu wa ofisi wa misaada ya kibinadamu kuhusu Gaza ameeleza kuwa oparesheni kubwa inahitajika ilikuwasilisha misaada katika Ukanda huo na kwamba hili haliwezi kufanyika wakati mapigano yakiendelea.

Aidha Andrea De Domenico amesema kuwa uharibifu wa miundo mbinu muhimu kama vile hosipitali, shule, nyumba za makaazi na vituo vya maji umeongeza changamoto kwa raia wa Gaza.

Zaidi ya raia wa Palestine milioni tatu wanahitaji msaada kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Zaidi ya raia wa Palestine milioni tatu wanahitaji msaada kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. REUTERS - IBRAHEEM ABU MUSTAFA

Afisa huyo pia ameeleza kuwa oparesheni iliomalizika ya wanajeshi wa Israeli katika hosipitali ya Shifa ambayo ni kubwa zaidi katika Ukanda wa Gaza, iliwacha kituo hicho kikiwa katika hali mbaya zaidi na kwamba ni vigumu kuendeleza shughuli zake.

Wito huu unakuja wakati huu ambapo Israeli imeahidi kufungua mipaka zaidi inayoingia katika Ukanda wa Gaza na kwamba itahakikisha kuwa misaada zaidi inaingia katika eneo hilo.

Hatua ya Israeli imekuja baada ya shambulio la ndege zisizo na rubani kusababisha vifo vya wahudumu saba wa shirika la misaada waliokuwa wanapeleka msaada katika Ukanda wa Gaza tarehe moja ya mwezi Aprili.

Raia wa Palestine wanaoishi katika kambi za wakimbizi katika eneo la Rafah, mpaka na Misri. Tarehe 10 Aprili 2024.
Raia wa Palestine wanaoishi katika kambi za wakimbizi katika eneo la Rafah, mpaka na Misri. Tarehe 10 Aprili 2024. © Mohammed Salem / Reuters

Mauaji ya wahudumu hao yalikashifiwa vikali na washirika wa karibu wa Israeli haswa wakati huu ambapo mapigano kati yake na Hamas yakiingia katika mwezi wa sita sasa.

Makabiliano kati ya pande hizo mbili yalianza baada ya wapiganaji wa Hamas kutekeleza shambulio baya zaidi kusini mwa Israeli ambapo karibia watu 1,200 waliuawa wengine 250 wakichukuliwa mateka.

Soma piaIsraeli yawashambulia tena Wapalestina waliokuwa wanasubiri msaada

Mashambulio ya Israeli ya kulipiza kisasi yamesababisha vifo vya zaidi ya raia 33,800 katika ukanda wa Gaza kwa mujibu wa takwimu za Hamas.

Hillary Ingati-RFI Kiswahili/AP

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.