Pata taarifa kuu

Miaka miwili ya mvua kwa saa 24: Shughuli zazorota Dubai kwa rekodi ya mvua

Falme za Kiarabu, mojawapo ya nchi kame zaidi duniani, imekumbwa na mvua kubwa iliyosababisha mafuriko, na kuua watu 18 katika jimbo jirani la Oman.


Falme za Kiarabu zimrekodi mvua ya miaka miwili ndani ya saa 24. Dubai, Aprili 17, 2024.
Falme za Kiarabu zimrekodi mvua ya miaka miwili ndani ya saa 24. Dubai, Aprili 17, 2024. AP - Jon Gambrell
Matangazo ya kibiashara

Barabara kuu zilizojaa maji na kusababisha mafuriko, shule zilizofungwa na kutatiza usafiri wa ndege na angalau mtu mmoja kufariki: shughuli zimezorota huko Dubai siku ya Jumatano kwa rekodi ya mvua iliyonyesha siku moja kabla kwenye majimbo saba ya miji maarufu ya shirikisho la Falme za Kiarabu. Nchi hiyo ya jangwa imerekodi mvua ya 254mm kwa siku moja, sawa na karibu miaka miwili ya mvua. Mvua hii katika Falme za Kiarabu ndiyo mvua kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa nchini humo tangu rekodi zilipoanza mwaka wa 1949, kulingana na mamlaka.

Maji yaliingia kila mahali: katika vituo vya ununuzi, hoteli za kifahari. Licha ya jua kirudi kuchomoza, mistari mirefu ilishuhudiwa kwenye barabara kuu za njia sita, ambazo sehemu zake zilikuwa bado zimeja maji. Baadhi ya nyumba zilikuwa bado hazina umeme, huku magari yaliyotelekezwa yakiendelea kuelea katika baadhi ya vitongoji ambavyo bado vimekuwa vimejaa maji. Mamlaka imetangaza kufungwa kwa shule wiki nzima, ikionyesha ugumu wa kurejea katika hali ya kawaida.

Hali tete

Baada ya afari nyingi za ndege kufutwa siku moja kabla, wasafiri walihimizwa wasisafiri hadi Uwanja wa Ndege wa Dubai, ulio na shughuli nyingi zaidi duniani katika masuala ya shughuli za kimataifa, "isipokuwa kama ni lazima kabisa." "Ndege zinaendelea kucheleweshwa na kuelekezwa kutua shehemu nzingine. Tunafanya kazi kwa bidii ili kurejesha utendakazi haraka iwezekanavyo katika mazingira magumu kabisa," amesema msemaji wa mamlaka ya viwanja vya ndege vya Dubai.

Shirika la ndege la Emirates, limesitisha ukaguzi kutokana na ugumu wa kufikia uwanja wa ndege kwa wafanyakazi na abiria, huku barabara zikiwa bado zimefungwa na baadhi ya huduma za metro zimesitishwa. Misururu mirefu imeonekana nje ya vituo vya teksi vya uwanja wa ndege, huku abiria wengi waliokuwa ndani wakisubiri habari za safari zao za ndege wakiwa wamechanganyikiwa kabisa.

Dhoruba hiyo ilipiga Falme za Kiarabu na Bahrain usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne, baada ya kuikumba Oman, nchi nyingine ya Ghuba, ambapo watu 18, wakiwemo watoto kadhaa, walifariki. 

Shule pia zitasalia kufungwa hadi wiki ijayo nchini Bahrain, ambayo ilirekodi mvua ya siku moja ya 96.88 mm siku ya Jumanne, kushinda 67.9 mm iliyorekodiwa mnamo 1995.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.