Pata taarifa kuu

Mashambulizi ya Iran: Nchi kadhaa ziliisaidia Israel kujilinda

"Shambulio la Irani lilizimwa, tulizuia 99% ya risasi kuelekea Israeli," msemaji wa jeshi la Israeli Aamesema kuhusu shambulio la kwanza la moja kwa moja kuwahi kutekelezwa na Jamhuri ya Kiislamu dhidi ya Israeli usiku wa Aprili 13 kuamkia 14. Ikiwa Israel iliweza kutegemea mifumo yake mbalimbali ya ulinzi kama Iron Dome, nchi kadhaa zilihusika katika kusaidia Tel Aviv kukabiliana na mashambulizi.

Mfumo wa ulinzi wa anga ukifanya kazi baada ya Iran kurusha ndege zisizo na rubani na makombora kuelekea Israel, ukionekana kutoka Ashkelon, Israel Aprili 14, 2024.
Mfumo wa ulinzi wa anga ukifanya kazi baada ya Iran kurusha ndege zisizo na rubani na makombora kuelekea Israel, ukionekana kutoka Ashkelon, Israel Aprili 14, 2024. REUTERS - Amir Cohen
Matangazo ya kibiashara

Mapema Jumamosi jioni, Joe Biden alitangaza kwamba vikosi vya Marekani vilisaidia kuangusha "karibu" ndege zisizo na rubani na makombora yote yaliyorushwa na Iran dhidi ya Israeli. "Kwa maelekezo yangu, kwa kusaidia ulinzi wa Israel, jeshi la Marekani limehamisha ndege na ndege za ulinzi wa makombora ya balestiki katika eneo hilo kwa muda wa wiki moja iliyopita," rais wa Marekani alitangaza. "Kupitia vikosi hivi na ustadi wa ajabu wa jeshi letu, tumesaidia Israeli kuharibu karibu ndege zisizo na rubani na makombora yote yanayokuja. " Mfumo wa ulinzi wa anga wa Marekani ulinasa ndege kadhaa zisizo na rubani zilizorushwa na Iran, vituo vya televisheni vya CNN na ABC viliripoti haswa, bila kutaja idadi ya ndege zilizodunguliwa au katika maeneo gani oparesheni hizi zilifanyika.

"Ufaransa ina teknolojia nzuri sana, ndege, rada - na najua kwamba zimechangia kushika doria katika anga," amesema Daniel Hagari, msemaji wa jeshi la Israeli, katika hotuba iliyoonyeshwa kwenye televisheni Jumamosi jioni, bila kutoa maelezo kamili kuhusu uwezekano wa ushiriki wa ndege za Ufaransa kuharibu makombora yaliyorushwa na Iran. Baadhi ya makombora 300 yalizinduliwa wakati wa shambulio hilo, "lakini kulikuwa na ulinzi bora wa anga wa IDF pamoja na Marekani, Uingereza, Ufaransa na nchi nyingine," msemaji huyo alisema. Ikihojiwa kuhusu suala hili na shirika la habari la AFP, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imesema "haiko tayari kutoa maoni".

"Ufaransa ilibidi kuchukua jukumu"

Ufaransa ilihakikisha "kujilinda" kwa vituo vyake vya Mashariki ya Kati wakati wa shambulio la Irani lililolenga Israeli, kutokana na "uwezo" wa ulinzi dhidi ya ndege, chanzo cha jeshi la Ufaransa kimesema siku ya Jumapili. "Tulichangia katika ufuatiliaji na ulinzi wa miundombinu ya kijeshi (kambi za jeshi) ambapo tumetumwa kwa njia za ulinzi," chanzo cha kijeshi cha Ufaransa kimeliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumamosi.

Kulingana na Jenerali Jean-Paul Palomeros, mkuu wa zamani wa makao makuu ya Jeshi la Wanahewa la Ufaransa na kamanda mkuu wa zamani wa NATO aliyehojiwa na RFI, "uwezekano mkubwa zaidi ni kwamba, kwa kweli, zikiwa kwenye kituo cha Jordan, ndege za Ufaransa zilihusika kukabiliana dhidi ya ndege zisizo na rubani, hasa ili kulinda kambi husika. Na kisha, bila shaka, kuchangia katika aina ya muungano kulinda Israeli. Rais alielezea hili kwa uwazi kwa kusema kwamba Israeli lazima ilindwe na nadhani kwamba Ufaransa lazima iwe na jukumu. "

Ufaransa iko kwenye kambi kadhaa huko Mashariki ya Kati, Jordan, Umoja wa Falme za Kiarabu na Iraq, na mara kwa mara hupeleka uwezo wa baharini na wa anga katika Bahari ya Mediterania ya Mashariki na karibu na Bahari Nyekundu. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron "alilaani kwa uthabiti mkubwa zaidi shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa lililozinduliwa na Iran dhidi ya Israel" na kutoa wito wa pande huika "kujizuia", katika ujumbe uliochapishwa Jumapili kwenye mdandao wa X.

"Vifaa vya kuruka" vilizuiliwa na Jordan

Jordan, jirani wa Israel, ilinasa "vifaa vya kuruka" vilivyoingia kwenye anga ya Jordan wakati wa shambulio lililozinduliwa na Iran, serikali ya Jordan ilisema katika taarifa. Jeshi la Jordan "litakabiliana na tishio au ukiukaji wowote unaohatarisha usalama wa nchi, raia wake, anga yake na eneo lake, popote linapotoka na kwa njia zote zinazopatikana", ilionya serikali. Taarifa kwa vyombo vya habari inabainisha kuwa wanajeshi "wamenasa na kuzima vifaa vilivyoingia kwenye anga yetu jana usiku", na kwamba mabaki yalianguka katika"maeneo kadhaa" bila kusababisha majeraha yoyote.

Uingereza pia imetoa msaada kwa Israel. "Tumetuma ndege kadhaa za ziada za Jeshi la Wanahewa la Kifalme na meli za mafuta za angani katika eneo hili," Wizara ya Ulinzi ilisema katika taarifa. "Ndege hizi za Uingereza zitazuia shambulio lolote la anga ndani ya safu ya misheni zetu zilizopo, ikiwa ni lazima," taarifa hiyo imeongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.