Pata taarifa kuu

Muafaka wa kusitisha vita kati ya Hamas na Israeli bado hujapatikana

Nairobi – Siku tatu za mazungumzo kati ya Israel na kundi la Hamas kuhusu usitishaji mapigano huko Gaza na kuachiliwa kwa mateka yameshindwa kufikia mafanikio, maafisa wa Misri wamesema, ikiwa ni chini ya wiki moja kabla ya kuanza kwa mwezi mtukufu wa Kiislamu wa Ramadhani.

Wapatanishi wanasema bado hawajakataa tamaa licha ya Hamas na Israeli kutofautiana kuhusu idadi ya watu watakobadilishana
Wapatanishi wanasema bado hawajakataa tamaa licha ya Hamas na Israeli kutofautiana kuhusu idadi ya watu watakobadilishana © Reuters - Kosay Al Nemer
Matangazo ya kibiashara

Haya yanajiri wakati huu, miezi mitano tangu vita kwenye eneo hilo ianze, imeacha sehemu kubwa ya Gaza kuwa magofu na kusababisha maafa makubwa ya kibinadamu, huku watu wengi, haswa katika eneo la kaskazini, wakihangaika kutafuta chakula.

Mashirika ya misaada yamesema imekuwa shida kupeleka vifaa na mahitaji mengine katika sehemu kubwa ya Gaza kwa sababu ya ugumu wa kuratibu na jeshi la Israel.

Marekani, Qatar na Misri zimetumia wiki kadhaa kujaribu kufikia makubaliano ambapo Hamas itawaachilia mateka hadi 40, huku Israel ikitarajiwa kuwaachilia baadhi ya wafungwa wa Kipalestina pamoja na kuruhusu misaada kufika Gaza.

Hata hivyo wapatanishi wanasema bado hawajakataa tamaa licha ya pande hizo kutofautiana kuhusu idadi ya watu watakobadilishana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.