Pata taarifa kuu

Gaza: 90% ya watoto chini ya miaka mitano ni wagonjwa, kulingana na Umoja wa Mataifa

Takriban asilimia 90 ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano huko Gaza wameathiriwa na ugonjwa mmoja au zaidi wa kuambukiza, kulingana na ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, Shirika la Afya Duniani (WHO) na shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) iliyotolewa siku ya Jumatatu.

Kusini mwa Ukanda wa Gaza, 5% ya watoto walio chini ya umri wa miaka miwili wanakabiliwa na utapiamlo mkali, kulingana na tathmini. "Kupungua kwa hali hiyo ya lishe ya watu katika miezi mitatu haijawahi kutokea ulimwenguni," mashirika hayo yamesema.
Kusini mwa Ukanda wa Gaza, 5% ya watoto walio chini ya umri wa miaka miwili wanakabiliwa na utapiamlo mkali, kulingana na tathmini. "Kupungua kwa hali hiyo ya lishe ya watu katika miezi mitatu haijawahi kutokea ulimwenguni," mashirika hayo yamesema. AP - Fatima Shbair
Matangazo ya kibiashara

 

"Watoto wenye njaa, waliodhoofika na walio na kiwewe kikubwa wana uwezekano mkubwa wa kuugua, na watoto wagonjwa, haswa wenye kuhara, hawawezi kunyonya virutubisho vizuri," mfanyakazi wa WHO amesema.

Wakati wa wiki mbili zilizotangulia tathmini hii, 70% ya watoto hao waliugua kuhara, mara 23 zaidi ikilinganishwa na hali ya mwaka 2022.

"Njaa na magonjwa ni mchanganyiko hatari," meneja wa dharura wa WHO Mike Ryan amesema katika taarifa. "Watoto wenye njaa, waliodhoofika na wenye kiwewe kikubwa wana uwezekano mkubwa wa kuugua, na watoto wagonjwa, haswa wale wanaohara, hawawezi kunyonya virutubisho vizuri," aliongeza.

Wiki 20 baada ya vita vya Israel dhidi ya Hamas, mashirika ya Umoja wa Mataifa yanasema chakula na maji safi yamekuwa "adimu sana" katika ardhi ya Palestina na karibu watoto wote wadogo wanaugua magonjwa ya kuambukiza.

"Ukanda wa Gaza unakaribia kushuhudia mlipuko wa idadi ya vifo vya watoto vinavyoweza kuzuilika, ambavyo vinaweza kuzidisha kiwango ambacho hakijaweza kuvumilika cha vifo vya watoto huko Gaza," amesema Ted Chaiban, naibu mkuu wa hatua za kibinadamu katika UNICEF katika Ukanda wa Gaza.

Kulingana na tathmini ya Umoja wa Mataifa, zaidi ya 15% ya watoto walio chini ya umri wa miaka miwili, au mmoja kati ya sita, wanakabiliwa na "utapiamlo mkali" kaskazini mwa Gaza, ambao umekosa kabisa misaada ya kibinadamu. "Kulingana na data zilizokusanywa mwezi Januari, hali huenda ikawa mbaya zaidi leo," mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaonya.

Kusini mwa Ukanda wa Gaza, 5% ya watoto walio chini ya umri wa miaka miwili wanakabiliwa na utapiamlo mkali, kulingana na tathmini. "Kupungua kwa hali hiyo ya lishe ya watu katika miezi mitatu haijawahi kutokea ulimwenguni," mashirika hayo yamesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.