Pata taarifa kuu

Ukanda wa Gaza wakumbwa na masambulizi makali, mawasiliano ya simu na intaneti yakatwa

Ikidhamiria kufanya vita vyake dhidi ya Hamas "hadi mwisho", Israel imeongeza mashambulizi ya anga siku ya Alhamisi, Desemba 14 katika Ukanda wa Gaza ambapo raia wanasalia katika hali mbaya zaidi. Marekani inamtuma mshauri wake wa usalama wa taifa mjini Jerusalem.

Moshi ukipanda juu baada ya mlipuko wa bomu huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Desemba 14, 2023.
Moshi ukipanda juu baada ya mlipuko wa bomu huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Desemba 14, 2023. © MAHMUD HAMS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika sasisho lililochapishwa kwenye mtandao wa X, shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limetangaza kwamba maeneo yaliyo karibu majengo yake kumejaa wakimbizi na watu wanaokabiliwa njaa na haina uwezo wa kutoa misaada kwa wale ambao hawakuweza kutoroka kuelekea kusini. 

Mamlaka ya Palestina yalaani kitendo cha jeshi la Israel 'kuchafua' msikiti

Mamlaka ya Palestina siku ya Alhamisi imeshutumu picha zinazowaonyesha wanajeshi wa Israel wakisoma sala ya Kiyahudi katika msikiti katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, wakiita "unajisi" huo "ni aibu".

Video hii, iliyopatikana na AFP, inawaonyesha wanajeshi wa Israel wakiwa ndani ya msikiti katika kambi ya wakimbizi ya Jenin, wakitumia vipaza sauti kukariri Shema Yisrael, sala kuu katika dini ya Kiyahudi. Mwishoni mwa video, vicheko vilisikika, wakati wanajeshi wakiondoka msikitini na wimbo wa Hanukkah ukirushwa hewani, kupitia kipaza sauti.

Msemaji wa Ofisi ya Rais wa Palestina, Nabil Abou Roudeina, amesema: "Kuvunjiwa heshima ya msikiti katika kambi ya Jenin na jeshi la Israel ni jambo la aibu na la kuchukiza" na dhidi ya "athari za mashambulizi haya". Ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa na Marekani "kuishinikiza Israel kukomesha ukiukaji wake dhidi ya watu wa Palestina, mali zao na maadili yao matakatifu."

Rais wa Uturuki Erdogan amuonya Joe Biden kuhusu athari ya kikanda ya mzozo huo

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amemuonya Rais wa Marekani Joe Biden siku ya Alhamisi jioni dhidi ya "athari mbaya ya kikanda na kimataifa" ya mzozo kati ya Israel na Hamas. Huu ulikuwa mkutano wa kwanza kati ya viongozi hao wawili tangu Oktoba 7. "Rais Erdogan amesema kwamba kuongezeka na kuongeza muda wa mashambulizi ya Israel kunaweza kuwa na matokeo mabaya ya kikanda na kimataifa," imebaini ikulu ya rais wa Uturuki katika taarifa iliyochapishwa kufuatia mazungumzo haya ya simu.

"Kuondolewa kwa usaidizi usio na masharti kutoka Marekani kwa Israel kunaweza kuhakikisha usitishaji wa haraka wa mapigano," Bw. Erdogan amesisitiza. Mshirika wa jadi wa Palestina, mkuu wa nchi ya Uturuki ameshutumu mara nyingi na kwa maneno makali operesheni za kijeshi za Israeli huko Gaza na uungaji mkono usio na masharti wa Marekani kwa Israeli, inayotajwa kama taifa la "kigaidi" na "kigaidi" linalojihusisha na mauaji ya kimbari”.

Washington inataka vita kati ya Israel na Hamas vikome "haraka iwezekanavyo"

Baada ya ziara ya Jake Sullivan, mshauri wa usalama wa Marekani mjini Jerusalem na mkutano wake na Waziri Mkuu wa Israel na Waziri wa Ulinzi, Yoav Gallant, afisa huyu wa Marekani ametangaza kwamba anataka vita kati ya Israel na Hamas vikome "haraka iwezekanavyo".

Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani Jake Sullivan amejadili wakati wa ziara yake nchini Israel leo mabadiliko "katika siku za usoni" ya mashambulizi ya Israel kwenye eneo la Gaza hadi "operesheni zisizo na nguvu", ameripoti msemaji John Kirby.

"Nadhani sote tunataka hili limalizike haraka iwezekanavyo," John Kirby pia amesema, akiongeza kwamba mzozo "unaweza kumalizika leo" ikiwa Hamas itaweka chini silaha zake, ambayo "haionekani kuwa na uwezekano kwa sasa."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.