Pata taarifa kuu

Israel yashambulia kwa makombora Gaza, raia wanaswa tena

Jeshi la Israel linashambulia tena kwa mabomu Ukanda wa Gaza Jumapili hii, Desemba 3, licha ya wito wa kimataifa wa kujizuia ili kuwalinda raia na katikati ya "mvutano" wa kuvunjika kwa usitishwaji wa mapigano na kundi la wapiganaji la Hamas.

Mama akiomboleza kifo cha binti yake aliyeuawa wakati wa shambulio la anga la Israeli katika Ukanda wa Gaza, huko Deir al Balah, Jumamosi, Desemba 2, 2023.
Mama akiomboleza kifo cha binti yake aliyeuawa wakati wa shambulio la anga la Israeli katika Ukanda wa Gaza, huko Deir al Balah, Jumamosi, Desemba 2, 2023. AP - Hatem Moussa
Matangazo ya kibiashara

 

Vikosi vya Ulinzi vya Israel vimeendelea kushambulia miundombinu ya Hamas huko Gaza usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa kitengo cha Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel. “Miongoni mwa miundombinu iliyokusudiwa ni mahandaki ya Hamas, kamandi za kivita za Hamas na maghala ya silaha. Kikosi cha mashambulizi kutoka Kikosi cha 7 cha Kivita cha jeshi la Israel kimewaua wapiganaji saba wa Hamas kwa kutumia ndege isiyo na rubani. Jeshi la Wanamaji la Israel limeendelea kushirikiana na vikosi vya ardhini na kuharibu miundombinu ya majini ya Hamas. "

Mwimbaji wa Canada The Weeknd atoa dola milioni 2.5 kwa Gaza

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limetangaza nia ya balozi mwema wa mpango huo, mwimbaji wa Canada The Weeknd, ambaye jina lake halisi ni Abel Tesfaye, kuchangia dola milioni 2.5 kwa Gaza. WFP imeeleza katika taarifa iliyotolewa kwamba kiasi hicho ni sawa na vifurushi milioni 4 vya chakula, ambavyo vitatoa chakula kwa Wapalestina 173,000 kwa muda wa wiki mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.