Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Iran kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na Misri

Maafisa kadhaa wa Iran walizungumza katika siku za hivi karibuni kuhusu kurejeshwa kwa uhusiano kati ya Iran na Misri baada ya zaidi ya miaka 40 ya kuvunjika kwa uhusiano wao, ishara ya Iran kurejea na kusikika katika ukanda huo.

Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei anakutana na Sultan Haitham bin Tareq wa Oman mjini Tehran, Iran, Mei 29, 2023. Ilikuwa ni katika hafla hiyo ambapo Ayatollah Ali Khamenei alisema anakaribisha kurejeshwa kwa uhusiano na Misri.
Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei anakutana na Sultan Haitham bin Tareq wa Oman mjini Tehran, Iran, Mei 29, 2023. Ilikuwa ni katika hafla hiyo ambapo Ayatollah Ali Khamenei alisema anakaribisha kurejeshwa kwa uhusiano na Misri. via REUTERS - WANA NEWS AGENCY
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Tehran, Siavosh Ghazi

Baada ya Saudi Arabia, Iran inakaribia kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na Misri. Uhusiano kati ya nchi hizo mbili ulivunjika baada ya mapinduzi ya Kiislamu ya 1979 na kutiwa saini kwa makubaliano ya amani kati ya Misri na Israel.

"Hatuna tatizo la nchi mbili," amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir Abdollahian.

Siku tatu zilizopita, Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, alisema wakati akimpokea Sultani wa Oman kwamba Tehran inakaribisha hatua ya kurejesha uhusiano wake na Misri.

Oman ni mpatanishi mkuu kati ya Tehran na Cairo.

Kurejeshwa kwa uhusiano kati ya Iran na Misri kutazidi kudhoofisha msimamo wa Marekani katika ukanda huo baada ya makabiliano kati ya Tehran na Riyadh.

Hii pia inawakilisha tishio kwa Israeli. Hakika, Iran inaunga mkono kifedha na kijeshi makundi ya Kiislamu ya Palestina na kuhalalisha uhusiano na Misri kunaweza kuwezesha msaada huu.

Iran inabaini kwamba imeibuka kuimarika kutokana na maendeleo haya, hasa kwa vile haijaacha chochote kuhusu sera yake ya kikanda, hasa kuhusu Syria au Yemen.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.