Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-HAKI

Iran yatangaza kuwa inataka kusamehe "idadi kubwa" ya waliopatikana na hatia na watuhumiwa

Iran imeamua kusamehe au kubatilisha vifungo vya jela kwa idadi kubwa ya wafungwa, hasa wale waliokamatwa tangu mwezi Septemba mwaka jana wakati wa maandamano ya upinzani dhidi ya mamlaka. Hatua hizi za huruma hazikuzuia kukamatwa kwa mwandishi mpya wa habari kutoka gazeti la kila siku la mwanamageuzi Ham Mihan.

Ayatollah Ali Khamenei tarehe 26 Novemba 2022 mjini Tehran.
Ayatollah Ali Khamenei tarehe 26 Novemba 2022 mjini Tehran. AP
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na vyombo vya habari vya serikali, hatua hizi za msamaha zinahusu makumi ya maelfu ya watu kati ya wale ambao wamehukumiwa vifungo au wale ambao wamekamatwa na bado hawajahukumiwa. Kiongozi Muadhamu wa Iran Ayatullah Ali Khamenei amekubali msamaha huo kabla ya maadhimisho ya miaka 44 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yatakayoadhimishwa Jumamosi Februari 11.

Hivyo, waliokamatwa kwa kuandika maneno ya kupinga serikali ukutani au kuwa na shughuli kwenye mitandao ya kijamii yenye chuki na Jamhuri wataachiwa mara moja na kesi yao itafungwa. Kupunguzwa kwa vifungo pia hutolewa kwa wafungwa.

Ishara kutoka kwa mamlaka

Maelfu ya watu walikamatwa kwa ushiriki wao katika vuguvugu la maandamano baada ya kifo cha Mahsa Amini mnamo mwezi Septemba 16, 2022. Alikamatwa kwa kutoheshimu uvaaji wa hijabula wa lazima kwa wanawake. Kulingana na maandishi yaliyochapishwa, wale watakaoachiliwa lazima watoe ahadi iliyoandikwa

Vile vile, watu wote wanaotuhumiwa au kuhukumiwa kwa uhusiano na idara za kijasusi za kigeni au kwa kuwashambulia au kuwaua askari wa vikosi vya usalama, kuchoma moto majengo ya umma au ni wanachama wa makundi yanayochukia Jamhuri ya Kiislamu wametengwa na hatua hizi za msamaha.

Bila shaka ni ishara kwa upande wa mamlaka kuwatuliza roho katika mkesha wa kumbukumbu ya ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu mnamo Februari 11 na mwaka mpya wa Iran, mwishoni mwa mwezi Machi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.