Pata taarifa kuu

Iran: Televisheni ya taifa yadukuliwa na picha ya Kiongozi Mkuu ikiteketea kwa moto

"Mwanamke, maisha, uhuru", kauli mbiu hii imekuwa ikisikika katika mitaa ya miji mingi nchini Iran kwa wiki tatu sasa. Maandamano ya watu wenye hasira yaliyoanzishwa baada ya kifo cha Mahsa Amini, mwanamke wa Kikurdi aliyekamatwa na polisi inayoheshimisha maadili mjini Tehran, na ambayo yanalenga utawala huo.

Kiongozi Mkuu Ayatollah Ali Khamenei, huko Tehran, Iran, Jumapili, Machi 21, 2021.
Kiongozi Mkuu Ayatollah Ali Khamenei, huko Tehran, Iran, Jumapili, Machi 21, 2021. AP
Matangazo ya kibiashara

Katika mikutano ya hadhara, waandamanaji mara nyingi huimba "kifo kwa dikteta". Na Jumamosi jioni, Oktoba 8, vuguvugu la upinzani lilifanikiwa kuvamia moja ya vituo vya televisheni ya kitaifa. Matangazo yalikatizwa kwa muda mfupi lakini, ilikuwa ujumbe mkubwa kwa waandamanaji.

Ilikuwa ni habari ya saa tatu usiku. Kituo cha televisheni ya IRINN ilikuwa katika habari na ikatangaza ripoti ya ziara ya Kiongozi mkuu wa Iran mjini Boushehr, kusini mwa nchi hiyo. Lakini kama picha zilivyoonyesha Ayatollah Ali Khamenei akihutubia mkusanyiko mdogo wa watu, matangazo yalikatizwa ghafla.

"Damu za vijana wetu zinatoka kwenye vidole vyako"

Badala ya hotuba ya Kiongozi mkuu wa Iranu, picha ya Ayatollah Ali Khamenei ilionekana ikiwa katikati ya miali ya moto. Na uso wa Kiongozi huyo wa  Iran ilionekana kwenye tundu la bunduki. Chini ya skrini, picha za wanawake wanne waliouawa katika wiki za hivi karibuni. Picha hizo, ambazo zinachochea maandamano, zinaambatana na sentensi mbili: "damu za vijana wetu zinachuruzika kutoka kwa vidole vyako. Ni wakati wa kuweka sawa vitu vyakoako (...) na ujitafutie mahali pengine pa kuishi familia yako nje ya Iran”.

Kundi lililodaiwa kutekeleza udukuzi huo linajiita “Adalat Ali”, au haki ya Ali. Haya yamewadia baada ya watu watatu kuuawa wakati waandamanaji walipokabiliana na maafisa wa usalama wakati wa maandamano ya kulalamikia mauaji ya Mahsa Amini.

Bi Amini alizuiliwa mjini Tehran na polisi wa kitengo cha uadilifu kwa madai kwamba hakufunika nywele yake ipasavyo.

Amin mwenye umri wa miaka 22 na ambaye ni wa jamii wa waKurdi alifariki siku tatu baada ya kukamatwa na mauaji yake yamesababisha wimbi jipya la maandamano nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.