Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Takriban watu 18 wauawa katika shambulizi dhidi ya msikiti mmoja nchini Afghanistan

Mlipuko mkubwa ulikumba moja ya misikiti mikubwa zaidi huko Herat, magharibi mwa Afghanistan, siku ya Ijumaa, na kuua watu 18 akiwemo imamu mashuhuri wa msikiti huo, ambaye wiki chache zilizopita alitoa wito wa kukatwa kichwa kwa yeyote anayetaka kuupinga utawala wa Taliban.

Mashambulizi mengi yalidaiwa kutekelezwa na IS, ambayo inalenga zaidi madhehebu ya Afghanistan ya Kishia, Sufi na Sikh, lakini pia Taliban.
Mashambulizi mengi yalidaiwa kutekelezwa na IS, ambayo inalenga zaidi madhehebu ya Afghanistan ya Kishia, Sufi na Sikh, lakini pia Taliban. Photo: RFI / Persian
Matangazo ya kibiashara

Picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha miili iliyotapakaa kwenye jengo la msikiti wa Gazaghah na vyombo vya habari vimesema vinahofia kuwepo na majeruhi wengi.

Mujib ur Rahman Ansari, mhubiri mashuhuri na mfuasi mkuu wa Taliban, ameuawa katika "shambulio la kikatili siku ya Ijumaa huko Herat", msemaji wa serikali Zabihullah Mujahid amethibitisha kwenye ukurasa wake wa Twitter. "Imarati ya Kiislamu inaeleza masikitiko yake makubwa kwa kifo chake na wale waliohusika na tukio hili wataadhibiwa kwa vitendo vyao viovu," ameahidi.

Shambulio hilo limesababisha vifo vya watu 18 na wengine 23 kujeruhiwa, kwa mujibu wa msemaji wa gavana wa jimbo la Herat.

Mujib ur Rahman Ansari aliwaangamiza waumini wengi na alijulikana kwa hotuba zake kali. Akizungumza katika mkutano wa viongozi wa kidini mjini Kabul mapema mwezi Julai, alisema mtu yeyote anayejaribu kuupindua utawala wa Taliban anapaswa kukatwa kichwa.

"Bendera hii (ya Taliban) haikupandishwa kirahisi, na haitashushwa kirahisi," alisema. "Wanazuoni wote wa kidini nchini Afghanistan wanapaswa kukubaliana (...) kwamba mtu yeyote anayefanya kitendo chochote dhidi ya serikali yetu ya Kiislamu akatwe kichwa na aangamizwe."

Idadi ya mashambulizi imepungua nchini Afghanistan tangu Taliban kuchukua mamlaka mwaka mmoja uliopita, lakini bado yanaendelea. Mashambulizi mengi yanadaiwa kutekelezwa na kundi la wanajihadi la Islamic State (IS). Mapema mwezi wa Agosti, kiongozi mwingine wa kidini wa Taliban na kaka yake waliuawa katika shambulio la bomu la kujitoa mhanga katika shule ya Qoran huko Kabul, shambulio liliodaiwa kutekelezwa na IS.

Kiongozi huyu, Rahimullah Haqqani, alijulikana hasa kwa shutma zake kali dhidi ya IS. Hivi majuzi alijitokeza hadharani akiunga mkono kuruhusu elimu ya wasichana nchini Afghanistan, ambapo shule za sekondari zimesalia kufungwa kwa wasichana wa shule tangu kurejea kwa Taliban madarakani.

Shambulio lingine la bomu katika msikiti wa Kabul wakati wa sala ya jioni mnamo Agosti 17 lilisababisha vifo vya watu 21. Msururu wa mashambulizi ya mabomu yaliikumba nchi hiyo hasa mwishoni mwa mwezi wa Aprili, wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, na mwishoni mwa mwezi Mei, ambapo makumi ya watu waliuawa. Mashambulizi mengi yalidaiwa kutekelezwa na IS, ambayo inalenga zaidi madhehebu ya Afghanistan ya Kishia, Sufi na Sikh, lakini pia Taliban.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.