Pata taarifa kuu

Wito wa fedha misaada za Umoja wa Mataifa wakabiliwa na upungufu mkubwa

Wito wa Umoja wa Mataifa wa kutaka fedha kwa ajili ya shghuli zao za kibinadamu unakabiliwa na upungufu mkubwa, Umoja wa Mataifa ulisema Ijumaa (tarehe 12 Agosti), ukionya juu ya hatari zinazoongezeka zinazowakabili wafanyakazi wa misaada.

Wito wa Umoja wa Mataifa unashughulikia hali kama vile ukame katika Pembe ya Afrika, matokeo ya vita vya Ukraine, Yemen (kwenye picha), Afghanistan na Syria.
Wito wa Umoja wa Mataifa unashughulikia hali kama vile ukame katika Pembe ya Afrika, matokeo ya vita vya Ukraine, Yemen (kwenye picha), Afghanistan na Syria. REUTERS - KHALED ABDULLAH
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Umoja wa Mataifa la kutoa misaada ya kibinadamu (OCHA) limesema wito wa Umoja wa Mataifa kwa programu zake za usaidizi duniani kote sasa unafikia dola bilioni 48.7 lakini ni dola bilioni 15 tu ambazo zimetolewa. "Mahitaji ya kimataifa hayajawahi kuwa makubwa kiasi hiki, huku kukiwa na rekodi ya watu milioni 303 walio katika hali mbaya duniani kote," msemaji wa OCHA Jens Laerke amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva.

Amebaini kwamba nakisi hii ya zaidi ya dola bilioni 33 ilikuwa "pengo kubwa zaidi ambalo hatujawahi kushuhudia (...) Hata hivyo, pia ni kiasi kikubwa zaidi cha fedha ambacho wafadhili wamewahi kutoa". "Kwa hiyo tatizo ni hili: mahitaji duniani kote yanaongezeka sana, kwa kasi zaidi kuliko fedha kutoka kwa wafadhili," ameongeza.

Wito wa Umoja wa Mataifa unashughulikia hali kama vile ukame katika Pembe ya Afrika, matokeo ya vita vya Ukraine, Yemen, Afghanistan na Syria.

Mazingira yakabiliwa na hatari zaidi

"Kuna nia ya kimataifa katika kushughulikia masuala haya kwa sababu mengi yao, yasiposhughulikiwa sasa, yataleta matatizo makubwa zaidi katika siku zijazo," Laerke ameongeza. Agosti 19 ni siku ya huduma za kibinadamu duniani, ambayo itaadhimishwa kwa sherehe katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko Geneva. "Kamwe kabla ya hapo wahudumu wa kibinadamu hawajaitwa kujibu kiwango kama hicho cha mahitaji, na wanafanya hivyo katika mazingira hatarishi," amesema Laerke.

Kwa mujibu wa takwimu za shirika lisilo la kiserikali la Humanitarian Outcomes, zaidi ya wafanyakazi 148 waliuawa wakiwa kazini mwaka jana, idadi kubwa zaidi tangu mwaka 2013. Tangu kuanza kwa mwaka huu, wafanyakazi wa misaada 168 walishambuliwa, na kusababisha vifo vya 44, kulingana na shirika la Humanitarian Outcomes.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.