Pata taarifa kuu

Tetemeko la ardhi nchini Afghanistan: Taliban yatoa wito wa kuwasaidia waathiriwa

Zoezi la kutafuta watu waliohai, miili ya nwatu waliofariki na majeruhi katika vifusi limekamilika nchini Afghanistan baada ya tetemeko la ardhi lililokumba eneo la kusini-mashariki mwa nchi hiyo usiku wa katikati mwa wiki hii.

Mtu huyu akiwa kwenye vifusi huko Gayan, katika mkoa wa Paktika, Juni 23, 2022, baada ya tetemeko la ardhi kupiga kusini mashariki mwa Afghanistan.
Mtu huyu akiwa kwenye vifusi huko Gayan, katika mkoa wa Paktika, Juni 23, 2022, baada ya tetemeko la ardhi kupiga kusini mashariki mwa Afghanistan. AP - Ebrahim Noroozi
Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya hivi punde inaripoti angalau makuni ya watu walioangamia. Waathiriwa wanakabiliwa na hali ya dharura.

Utawala wa Taliban, ukiwa unakabiliwa na hali ngumu, unatoa wito kwa msaada kutoka jumuiya ya kimataifa kutokana na ukubwa wa uharibifu - nyumba 1,500 zilizoharibiwa au kusombwa na maji - na watu wanahitaji msaada wa kutosha.

Saa 48 baada ya tetemeko kubwa la ardhi katika kipindicha miaka ishirini iliyopita nchini Afghanistan, wakazi wa jimbo la Paktika wameshushwa asubuhi ya leo na tetemeko jipya, tetemeko ndogo. Mara mbili, ardhi imetetemeka kwa sekunde chache.

Mitetemeko, nyepesi, haina uhusiano wowote na ghasia za kile ambacho raia waliweza kushuhudia siku mbili zilizopita katika jimbo hili. Lakini ni katika muktadha huu ambapo mamia ya wanakijiji ambao wamepoteza nyumba zao za udongo, tangu zilipoporomoka Jumatatu jioni.

Wanakijiji wanalala nje, bila chakula, maji, blanketi na makazi ya dharura kwa vile usiku kunaripotiwa baridi kali. Kusaidia watu hawa waliokumbwa na maafa sasa ni suala la dharura. Lakini kutoa misaada ni changamoto katika maeneo haya ya milima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.