Pata taarifa kuu

Mfahamu Ayman al-Zawahiri, mrithi wa bin Laden kama mkuu wa al-Qaeda

Akiwa mkuu wa al-Qaeda tangu kifo cha Osama bin Laden, Mmisri Ayman al-Zawahiri, ambaye kifo chake kilitangazwa Jumatatu na Joe Biden, alitoa nadharia ya kuzuka kwa makundi ya wanajihadi bila ya kuwadhibiti.

Mmisri, Kiongozi wa al-Qaeda Ayman al-Zawahiri (kulia), hapa akiwa  pamoja na Osama bin Laden mwaka 2001, aliuawa na shambulio la ndege zisizo na rubani za Marekani zilizomlenga mjini Kabul.
Mmisri, Kiongozi wa al-Qaeda Ayman al-Zawahiri (kulia), hapa akiwa pamoja na Osama bin Laden mwaka 2001, aliuawa na shambulio la ndege zisizo na rubani za Marekani zilizomlenga mjini Kabul. REUTERS/Hamid Mir
Matangazo ya kibiashara

Kama mmoja wa wabunifu wa mashambulizi ya Septemba 11, 2001, "mafanikio makubwa zaidi ya Zawahiri ni kkuliendeleza kundi la Al-Qaeda", kulingana na Barak Mendelsohn, profesa katika Chuo Kikuu cha Haverford huko Pennsylvania. Lakini ilimbidi kuzidisha "faradhi" na kujiunga kwa makundi mengi kwa kundi hili, kutoka Rasi ya Uarabuni hadi Maghreb, kutoka Somalia hadi Afghanistan, Syria na Iraq. Na kukiri kwamba wameanza kujizatiti kidogo kidogo.

Kiongozi huyo mwenye ndevu ndefu na miwani mikubwa, anayetambulika kwa urahisi kwa nundu kwenye paji la uso, alijiunga na Muslim Brotherhood akiwa na umri wa miaka 15. aliendesha harakati za kijiadi kwa miaka 40, kabla ya kuuawa akiwa na umri wa miaka 71 katika shambulio la ndege isiyo na rubani.

Alipotangazwa kuwa amekufa au kufariki mara kadhaa, hivi karibuni alikonekana kuwa na ishara za kuishi kwa muda mrefu. "Al-Zawahiri alionekana kuwa na uwezo wa kupata umaarufu mkubwa kwa wafuasi wake baada ya kundi la Taliban kuchukuwa madaraka nchini Afghanistan," kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa katikati ya mwezi wa Julai.

Marekani ilitoa dola milioni 25 kwa kukamatwa kwake. Alikuwa ni kero kwa Marekani hadi tangazo la rais wa Marekani binafsi kuhusu kifo chake, wakati wa "operesheni ya kupambana na ugaidi" wikendi hii.

Kutoka Muslim Brotherhood hadi Al-Qaeda

Alizaliwa Juni 19, 1951 huko Maadi, karibu na Cairo, katika familia ya kitajiri - baba yake alikuwa daktari maarufu na babu yake mwanatheolojia mkuu wa msikiti wa al-Azhar katika mji mkuu wa Misri -, Ayman al-Zawahiri alikuwa daktari wa upasuaji.

Akihusishwa na mauaji ya 1981 ya Rais wa Misri Anouar al-Sadat, alifungwa kwa miaka mitatu, kisha akajiunga na Saudi Arabia na Pakistani katikati ya miaka ya 1980 ambapo aliwatibu wanajihadi waliokuwa wakipigana na Urusi ya zamani na kukutana na Bin Laden.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.