Pata taarifa kuu
IRAN-USHIRIKIANO

Ali Khamenei ataka kurejelewa upya kwa makubaliano ya kurejesha uhusiano na Israeli

Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amezitaka nchi za Kiarabu zilizorejesha uhusiano na Israel kurejelea uamuzi wao na kuvunja mara moja uamuzi huo, akibaini kwamba nchi hizo  zilifanya madhambi makubwa.

Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei.
Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei. AP
Matangazo ya kibiashara

Mataifa ya Kiarabu ambayo yalifufua uhusiano na Israeli mnamo mwaka 2020 lazima yabadilishe maamuzi yao, Kiongozi Mkuu wa Irani Ali Khamenei amesema katika hotuba yake Jumapili (Oktoba 24) wakati wa hafla ya Waislamu huko Tehran.

"Kwa bahati mbaya, serikali baadhi ya zimefanya makosa, makosa makubwa na dhambi katika kuanzisha tena (uhusiano wao) na utawala wa Kizayuni unaojihusisha na dhulma na uonevu, akimaanisha Israel.

Ni kitendo dhidi ya umoja wa Kiisilamu, lazima wafikirie upya na kujutia kosa hili kubwa, ”Khamenei amesema, kulingana na hotuba yake iliyorushwa kwenye runinga ya serikali, shirika la habari la AFP limeripoti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.