Pata taarifa kuu
LEBANON-SIASA

Najib Mikati ateuliwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Lebanon

Mfanyabiashara Najib Mikati ameteuliwa kuwa Waziri Mkuu baada ya kuungwa mkono na wabunge wengi leo Jumatatu wakati wa mashauriano juu ya uteuzi wa waziri mkuu mpya nchini Lebanon.

Rais wa Lebanon Michel Aoun (kulia) akikutana kwa mazungumzo na Waziri Mkuu mpya Najib Mikati katika ikulu ya Baabda, baada ya kuteuliwa kushikilia wadhifa huo Julai 26, 2021.
Rais wa Lebanon Michel Aoun (kulia) akikutana kwa mazungumzo na Waziri Mkuu mpya Najib Mikati katika ikulu ya Baabda, baada ya kuteuliwa kushikilia wadhifa huo Julai 26, 2021. . DALATI AND NOHRA/AFP
Matangazo ya kibiashara

Najib Mikati, ambaye tayari ameshikilia wadhifa wa kiongozi wa serikali mara mbili na hatoki katika chama cha cha kisiasa au muungano wowote wa kisiasa, ameidhinishwa kwa kura 73 kwa jumla ya wabunge 118.

Najib Mikati ambaye tayari anaungwa mkono na kundi la mawaziri wakuu wa zamani wa Lebanon, pia Jumatatu hii amepata uungwaji mkono kutoka Hezbollah, chama cha kishia chenye silaha ambacho Marekani inakichukulia kama kundi la kigaidi.

Vyama vingi vikuu vyenye viti bungeni pia vimeunga mkono uteuzi huu, pia anaungwa mkono na Saad Hariri, aliyeteua kuwa Waziri Mkuu mwezi Oktoba mwaka iliyopita lakini ambaye alijiuzulu katikati ya mwezi Julai baada ya kushindwa kuunda serikali kwa sababu ya kutokubaliana na rais Michel Aoun, kulingana Bw. Hariri.

Lebanon, iliyotawala kwa karibu mwaka mmoja na serikali ya mpito iliyoteuliwa baada ya mlipuko mkubwa mbaya ulioharibu bandari ya Beirut mnamo Agosti 4, inakabiliwa na kuporomoka kwa sarafu, ukosefu wa ajira na akaunti za benki kuzuiwa, uchumi wa nchi kudorora - huku ikiwa moja ya nchi zenye madeni makubwa ulimwenguni - na hivyo kukumbwa na mgogoro mkubwa kabisa tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 1975-90.

Katika mfumo wa kisiasa wa Lebanoni, wadhifa wa Waziri Mkuu lazima uchukuliwe na Mwislamu kutoka dhehebu la Sunni, wakati nafasi ya rais nashikiliwa na Mkristo wa Kimaroni.

Nchi za Magharibi zimeongeza shinikizo kwa Lebanon kuwezesha uundaji wa serikali ambayo inaweza kufanya marekebisho ya serikali iliyoathiriwa na ufisadi, haswa zikitishia kuweka vikwazo na kuzuia msaada wa kifedha maadamu mageuzi hayatakuwa yameanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.