Pata taarifa kuu
LEBANON-SIASA-USALAMA

Lebanon: Saad Hariri ateuliwa tena kuwa waziri mkuu ili kuunda serikali mpya

Baada ya mashauriano katika bunge yakiongozwa na rais Michel Aoun, Saad Hariri ameteuliwa tena kuwa Waziri Mkuu wa Lebanon. Atalazimika kufikia makubaliano na vyama mbalimbali vya siasa katika nchi hiyo ili kuunda serikali yenye uwezo wa kutekeleza mageuzi muhimu ili kuiondoa Lebanon kwenye mgogoro unaoikabili.

aad Hariri katika mkutano na waandishi wa habari huko Uholanzi, Agosti 14, 2020.
aad Hariri katika mkutano na waandishi wa habari huko Uholanzi, Agosti 14, 2020. REUTERS/Piroschka Van De Wouw/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Saad Hariri amechaguliwa na wabunge wengi, 65, kulingana na taarifa iliyosomwa kwenye mkutano na waandishi wa habari na afisa mwandamizi wa katika ofisi ya rais.

Saad Hariri anachikilia wadhifa wa waziri mkuu nchini Lebanon mara tatu mwaka 2009-2011 na kisha kuanzia mwaka 2016, alishikilia wadhifa huo. Siku yake ya mwisho kushikilia wadhifa huo ilikuwa tarehe 29 Oktoba, 2019, baada ya kujiuzulu kufuatia shinikizo la maandamano ambayo haijawahi kutokea katika historia ya hivi karibuni ya nchi hiyo.

Anarejea kushikilia wadhifa huo wakati waandamanaji wanaendelea kumiminika mitaani wakidai viongozi wapya kwenye uongozi wa nchi, na mabadiliko ya jumla katika mfumo wa uongozi wa nchi kwa miezi. Mtangulizi wake, Moustapha Adib, ambaye alikuwa ameteuliwa Agosti 31, alijiuzulu kwenye nafasi hiyo mwezi mmoja baadaye bila kuweza kupatia suluhu uhasama kati ya vyama vya siasa.

Lebanon inapitia mgogoro mkubwa wa kisiasa na kiuchumi na iliathirika zaidi na mlipuko wa Agosti 4 huko Beirut, ambapo wanasiasa walinyooshewa kidole cha lawama.

Tangu kutokea kwa janga hili, viongozi wa Lebanon wamekuwa chini ya shinikizo kutoka kwa jamii ya kimataifa, hasa Ufaransa, kutafuta suluhisho la kumaliza mgogoro huo. Lakini vyama viligawanyika na muda mwingi ulipotea.

Hakuna uhakika kwamba kurejea kwa Saad Hariri kama waziri mkuu kutawaridhisha wananchi wa Lebanon. Saad Hariri ameahidi kwa upande wake kuundwa kwa "serikali ya wataalam" kwa"jitihada za Ufaransa" na amejikubalisha "kuunda serikali haraka, kwa sababu wakati unakwisha na nchi inakabiliwa na nafasi yake ya pekee na ya mwisho".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.