Washington yaipunguzia misaada Afghanistan kutokana na mvutano wa kisiasa
Marekani imetangaza kwamba itapunguza dola bilioni 1 kwa msaada iliyokuwa ikiitolea Afghanistan, na iko tayari kufanya vivyo hivyo mnamo mwaka 2021 baada ya rais wa Afghanistan Ashraf Ghani na mpinzani wake Abdullah Abdullah kushindwa kuunda serikali mpya.
Imechapishwa:
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo amethibitisha taarifa hiyo na kubaini kwamba Marekani ilikuwa na matumani kwamba Afghanistan sasa inaelekea pazuri
Ashraf Ghani na Abdullah Abdullah wote walidai kuwa walishinda uchaguzi uchaguzi wa urais uliofanyika Septemba 28, ambao uligubikwa na tuhuma za udanganyifu, matatizo ya kiufundi na vurugu.
"Pia tutaanza kutathmini programu zetu na miradi yetu yote ili kupunguza zaidi misaada yetu kwa Afghanistan na tutafikiria tena ahadi zetu kwa minajili ya mikutano ya wafadhili ijayo kwa Afghanistan," imesema taarifa ya Pompeo iliyotolewa baada ya mazungumzo yaliyofanyika huko Kabul.