Pata taarifa kuu
ISRAELI-SIASA-USALAMA

Israeli: Benjamin Netanyahu ashinda uchaguzi wa ndani ya chama cha Likud

Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, anayekabiliwa na mashitaka kwa zaidi ya mwezi mmoja kwa makosa ya ufisadi, amejitangaza leo Ijumaa, Desemba 27, mshindi wa uchaguzi uliofanyika jana Alhamisi ndani ya chama chake cha Likud.

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu aahidi wafuasi wa chama cha Likud kuwa watapata 'ushindi mkubwa katika uchaguzi ujao'. (picha ya kumukumbu)
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu aahidi wafuasi wa chama cha Likud kuwa watapata 'ushindi mkubwa katika uchaguzi ujao'. (picha ya kumukumbu) REUTERS/Ammar Awad
Matangazo ya kibiashara

"Ushindi mkubwa! Asante kwa wanachama wa Likoud kwa ujasiri wao, uungwaji wao mkono na mapenzi yao, "Benjamin Netanyahu ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter saa moja baada ya kumalizika kwa uchaguzi, ambapo matokeo ya awali yalikuwa yalimpa ushindi mwembamba dhidi ya mpinzani wake Gideon Saar.

'Kwa msaada wenu na ule wa Mungu, nitaongoza chama cha Likud kwa lengo la kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi ujao na tutaendelea kuendeleza taifa la Israeli kwa mafanikio ambayo haijawahi kupata,' ameongeza Benjamin Netanyahu.

Baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa saa tano usiku, Gideon Saar, Waziri wa zamani wa Benjamin Netanyahu na mbunge, aliwashukuru wafuasi wake na wapiga kura. Wabunge 57,000 walipiga kura katika uchagui huo ambao uliombwa na Gideon Saar baada ya Benyamin Netanyahu kushtakiwa mwezi uliopita kwa makosa ya ufisadi na kosa la udanganyifu katika kesi tatu.

Benjamin Netanyahu, ambaye anaongoza chama cha Likud tangu mwaka 1993 amefutilia mbali 'madai ya uwongo yanayochochewa na mambo ya kisiasa'.

Bw Netanyahu sasa ana kazi kubwa ya kuongoza kampeni ya chama cha Likud kwa uchaguzi wa wabunge mwezi Machi, uchaguzi wa tatu chini ya mwaka mmoja.

Baada ya uchaguzi wa mapema mwezi Aprili na Septemba, Benyamin Netanyahu na Benny Gantz, kiongozi wa muungano wa chama cha mrengo wa kati Blue and White alliance walishindwa kupata idadi ya viti ya 61bungeni, ili kuunda serikali. Rais Reuven Rivlin alilazimika kukabidhi kazi hii kwa Bunge lenyewe, ambalo pia halikufanikiwa, na hivo kupelekea uchagui mqengine kufanyika katika nchi hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.