Pata taarifa kuu
UTURUKI-SYRIA-MAREKANI-USALAMA

Uturuki: Tumekamilisha maandalizi ya kuivamia Syria

Siku moja baada ya Rais wa Marekani kusema kuwa nchi yake injiandaa kuondoka Kaskazini mwa Syria kupisha jeshi la Uturuki kuanzisha operesheni ya kijeshi, serikali ya Uturuki imesema maandalizi ya kushambulia eneo la kaskazini mwa Syria yalikwishakamilika.

Kikosi cha Wanajeshi wa Uturuki kaskazini mashariki mwa Afrin, Syria, Januari 23, 2018.
Kikosi cha Wanajeshi wa Uturuki kaskazini mashariki mwa Afrin, Syria, Januari 23, 2018. REUTERS/Khalil Ashawi
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo uamuzi wa trump umekosolewa na wengi nchini Marekani ikiwa ni pamoja na viongozi vigogo wa chama cha Republican serikalini, huku wakitilia mashaka hatua ya jeshi ya Uturuki dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi ambao ni washirika wa Marekani katika vita dhidi ya kundi la Islamic State.

Vigogo hao kutoka chama cha Republican wanabaini kwamba ikiwa askari wa Marekani wataondoka kwenye mpaka na Uturuki na kuachia jeshi la Uturuki kuendesha operesheni katika eneo hilo la mpakani, kuna hatari jeshi hilo kushambulia waiganaji wa Kikurdi wanashirikiana na Marekani katika vita dhidi ya Islamic State.

Seneta wa Marekani Lindsey Graham na mshirika wa karibu wa Rais Donald Trump amesema huenda akaiitisha bunge la Congress ili libatilishe uamuzi wa Rais wa Marekani wa kuondoa vikosi vya Marekani kutoka katika mpaka wa Syria na Uturuki.

Lindsey Graham ambaye ni mwenyekiti wa kamati sheria katika bunge la Congress ameuelezea uamuzi wa Rais Trump wa kuondoa wanajeshi wake katika mpaka huo kama janga kwa Marekani, raia wa Syria na washirika wake wapiganaji wa Kikurdi.

Lindsey Graham ameongeza kusema kuwa hatua ya kuondoa wanajeshi wa Marekani ni kuwatenga wapiganaji wa Kikurdi ambao walikua washirika wakubwa wa Marekani katika harakati za kulisambaratisha kundi la wapiganaji wa kijihadi, Islamic State.

Kwa upande wake Serikali ya Uturuki kupitia kwa Rais Recep Tayyip Erdogan imesema itaanzisha operesheni ya kujilinda dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi kama walivyokubaliana na Rais Trump kwa njia ya simu huku wakidai kuwa wapiganaji wa kikurdi ni magaidi.

Umoja wa Ulaya umeonya kuwa hatua zinazotaka kuchukuliwa na Uturuki za kukabiliana na Wakurdi zitahatarisha usalama wa raia nchini Syria na Uturuki yenyewe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.