Pata taarifa kuu
SAUDI ARABIA-MAREKANI-UCHUNGUZI

Khashoggi: Riyadh yafutilia mbali msimamo wa bunge la Seneti la Marekani

Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia imefutilia mbali 'msimamo wa hivi karibuni wa bunge la Seneti la Marekani" kuhusu mauaji ya mwandishi wa habari wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi, ambaye aliuawa katika ubalozi mdogo wa nchi hiyo mjini Istanbul tarehe 2 Oktoba.

Mwanamfalme wa Saudi Arabia, Mohammed ben Salman.
Mwanamfalme wa Saudi Arabia, Mohammed ben Salman. REUTERS/Faisal Al Nasser
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia inasema kuwa uhalifu huo hauendani kabisa na sera za utawala wa kifalme.

"Saudi Arabia inafutilia mbali msimamo uliotolewa na bunge la Seneti la Marekani ambalo kupitia habari zisizokuwa na msingi na ambazo zinaingilia kati katika masuala ya ndani ya nchi hii, kudhoofisha jukumu lake katika kanda na kimataifa," imesema taarifa ya wizara hiyo iliyochapishwa na shirika la Habari la Saudia.

"Tangu awali Saudi Arabia imehakikishia kwamba mauaji ya raia wa Saudia Jamal Khashoggi ni uhalifu mbaya ambao hauendani na sera ya utawala wa kifalme au taasisi zake."

Siku ya Alhamisi bunge la Seneti la Marekani lilimtaka Rais Donald Trump kutambua Mwanamfalme wa Saudi Arabia kuwa alihusika katika mauaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi na kupigia kura azimio ambalo linaomba kusitishwa misaada ya kijeshi kwa utawala wa Saudi Arabia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.