Pata taarifa kuu
YEMEN-USALAMA

Watu 150 wauawa Yemen

Watu 150 wameripotiwa kuuawa katika kipindi cha saa 24 kutokana na mapigano yanayoendelea kushuhudiwa nchini Yemen kwenye mji wa Hodeida, mauaji ambayo yanaripotiwa wakati huu kukiwa na shinikizo la kimataifa la kutaka kuwepo kwa usitishwaji wa mapigano.

Vikosi vya serikali vikipiga kambi katika mji wa Hodeida Novemba 10, 2018.
Vikosi vya serikali vikipiga kambi katika mji wa Hodeida Novemba 10, 2018. Khaled Ziad / AFP
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya serikali vinavyosaidiwa na nchi washirika na Saudi Arabia wanapigana kujaribu kuwafurusha wapiganaji waasi wa Huthi wanaosaidiwa na Serikali ya Iran.

Vikosi vya Serikali na nchi washirika wamezidisha mashambulizi kwenye mji huo muhimu wa bandari kwa lengo la kuurejesha kwenye himaya yao.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya kuhusu uwezekano wa kutokea kwa janga la kibinadamu ikiwa mapigano hayatakoma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.