Pata taarifa kuu
ISRAELI-SYRIA-USALAMA

Netanyahu: Israeli haitawapokea wakimbizi kutoka Syria

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema raia wa Syria wanaokimbilia nchini humo kwa sababu ya vita nchini mwao, hawataruhusiwa kuingia nchini Israeli.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. REUTERS/Ronen Zvulun
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, Netanyahu amesema serikali yake itaendelea kutoa misaada ya kibinadamu kwa raia wa Syria wanaoendelea kuteseka.

Netanyahu amesisitiza kuwa, serikali yake imechukua hatua hii kwa sababu za kiusalama.

Wakati huo huo mazungumzo yamerejelewa tena kati ya wapinzani wa Syria na wajumbe wa Urusi, ili kupata mwafaka wa kusitisha mapigano katika ngome ya upinzani Kuisni Magharibi mwa nchi hiyo.

Wajumbe wa pande zote mbili wamekuja baada ya watu 75 wakiwemo watoto 23 kuuawa baada ya kushgambuliwa na wanajeshi wa serikali ya Syria wakisaidiwa na wale wa Urusi.

Mazungumzo haya yamekuja baada ya wajumbe kushindwa kuelewana siku ya Jumamosi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.