Askari 30 wa Afghanistan wauawa na Taliban
Askari thelathini wa Afghanistan wameuawa Jumatano wiki hii katika shambulio la kuvizia la Taliban katika jimbo la Magharibi la Badghis, gavana wa jimbo hilo amesema.
Imechapishwa:
Hili ni shambulio la kwanza kubwa la Taliban lililogharimu maisha ya askari wengi wa Afghanistan tangu kutangazwa kusitishwa mapigano kwa muda wa siku tatu, siku ya Jumapili, kutokana na sherehe za Eid el Fitr.
Majeshi ya Serikali pia yasitisha mapigano. Muda huo ungelimalizika leo Jumatano, lakini serikali ya Afghanistan ilikua iliongeza siku kumi.
Wapiganaji wa Taliban waliruhusiwa kushiriki mwishoni mwa wiki iliyopita katika sherehe za kumaliza mwezi mtukufu wa Ramadhan katika miji kadhaa ya Afghanistan.