Pata taarifa kuu
MAREKANI-ISRAEL-PALESTINA-USALAMA

Kiongozi wa Al Qaeda atangaza jihad dhidi ya Marekani

Kiongozi wa Al Qaeda, Ayman al-Zawahiri, ametoa wito wa vita takatifu (jihad) dhidi ya Marekani, akisema uamuzi Washington wa kuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem ni ushahidi kwamba Wapalestina wanafanyiwa unyonge.

Waandamanaji wakikusanyika kwenye kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Nakba na dhidi yahatua ya MArekani ya kuhamisha ubalozi wake Jerusalem, Suwaimah, Mei 11, 2018.
Waandamanaji wakikusanyika kwenye kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Nakba na dhidi yahatua ya MArekani ya kuhamisha ubalozi wake Jerusalem, Suwaimah, Mei 11, 2018. REUTERS/Muhammad Hamed
Matangazo ya kibiashara

Katika video ya dakika tano inayoanza na maneno "Tel Aviv pia ni nchi ya Waislamu," Ayman al-Zawahiri ,daktari kutoka Misri, ambaye alichukua uongozi wa Al Qaeda baada ya kifo cha mwanzilishi wake Osama Bin Laden, aliyeuawa mnamo mwaka 2011, ameita Mamlaka ya Palestina kuwa ni "wauzaji wa Palestina" na kuwataka wafuasi wake kuchukua silaha dhidi ya Marekani.

Rais wa Marekani Donald Trump "alikuwa muwazi na amefichua vita vya kidini vya kisasa (...). Hakuna kushirikian naye, ispokua kukabiliana na hali hii ya dhulma (...) kwa njia ya jihad "Ayman al-Zawahiri amesema, kwa mujibu wa nakala iliyotolewa na tovuti ya Intelligence Group, shirika maalumu linalofuatilia mitandao ya makundi ya Kiislam.

Ayman al-Zawahili amesema nchi za Kiislamu zimeshindwa kuchukua hatua kwa maslahi ya Waislamu kwa kutii Umoja wa Mataifa, taasisi inayotambua Israel na kutii maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa badala ya Sharia (sheria za Kiislamu ).

Maelfu ya raia wa Israel waliandamana siku ya Jumapili katika mitaa ya Jerusalem wakionyesha furaha yao baada ya Marekani kuchukua hatua ya kuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem.Mapema Jumatatu asubuhi kumezuka vurugu katika mji wa Jerusalem karibu na eneo ambako kumehamishiwa ubalozi wa Marekani. raia wa Palestina wamekabiliana na polisi ya Israel. Watu kadhaa wamekamatwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.