Pata taarifa kuu
SYRIA-USALAMA

Watu zaidi ya 35 wauawa katika mashambulizi Syria

Watu zaidi ya 35 walmeuawa leo Jumanne katika mashambulizi dhidi ya ngome ya waasi karibu na mji mkuu wa Syria, Damascus. Hayo yanajiri wakati ambapo serikali ya Syria imeendelea kushtumiwa kufanya mashambulizi ya kemikali.

Majengo yakiharibiwa na mashambulizi katika jimbo linalozingirwa la Ghouta mashariki, Syria.
Majengo yakiharibiwa na mashambulizi katika jimbo linalozingirwa la Ghouta mashariki, Syria. REUTERS/Bassam Khabieh
Matangazo ya kibiashara

Katika suala la kibinadamu, Umoja wa Mataifa unataka "mapigano yakomeshwe mara moja" kwa muda wa mwezi kwa kuruhusu misaada kwa raia wanaozingirwa kwa miezi kadhaa na jeshi la serikali.

Jeshi la Syria limelenga ngome ya waasi ya Ghouta mashariki, shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH), limeripoti. Kwa mujibu wa shirika hilo watoto watatu ni miongoni mwa waathirika wa mashambulizi hayo yaliyowajeruhi watu zaidi ya 160.

Idadi ya watu waliopoteza maisha inaweza kuongezeka kutokana na kuepo kwa watu waliokwama chini ya vifusi, ambao wako katika hali mbaya, Mkurugenzi wa OSDH, Rami Abdel Rahman, ameliambia shirika la habari la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.