Zaidi ya watu 300 wakamatwa nchini Uturuki
Uturuki imetangaza leo Jumatatu kwamba imewakamatwa watu zaidi ya 300 ambao wamekosoa kwenye mitandao ya kijamii jeshi la nchi hiyo kuzindua mashmabulizi kaskazini magharibi mwa Syria.
Imechapishwa:
Tangu kuzuka kwa operesheni iliyoitwa "Mazao ya Zabibu" dhidi ya wanamgambo wa Kikurdi katika eneo la Afrin, mamlaka ya Uturuki imeonya kwamba itawashughulikia wanaopinga, wanaokosoa au kupotosha utaratibu wa jeshi kuingilia kati.
Katika taarifa iliyotolewa leo Jumatatu, wizara ya mambo ya ndani imesema kuwa watu 311 walifungwa siku hizi 10 zilizopita kwa"kueneza propaganda ya kigaidi".
Uturuki inawachukulia wanamgambo wa Kikurdi YPG kama kundi la kigaidi na vuguvugu la chama cha PKK, ambalo lilichukua silaha nchini Uturuki mnamo mwaka 1984.