Pata taarifa kuu
IRAN-IRAQ-TETEMEKO-MAJANGA

Iran yapata hasara kubwa kufuatia tetemeko la ardhi

Kwa mujibu wa takwimu rasmi za mwisho, watu 407 wapoteza maisha na zaidi ya 7000 kujeruhiwa katika tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa digrii 7.3 kwa kiwango cha Richter lililopiga mkoa wa Kermanshah magharibi mwa Iran. Shughuli za uokoaji zinaendelea kujaribu kutafuta waathirika chini ya vifusi.

Wakazi wa jiji la Iran la Sarpol-e Zahab, mkoani Kermanshah, karibu na mpaka wa Iraq, Novemba 13, 2017.
Wakazi wa jiji la Iran la Sarpol-e Zahab, mkoani Kermanshah, karibu na mpaka wa Iraq, Novemba 13, 2017. Farzad MENATI / TASNIM NEWS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Watu zaidi ya 300 walipoteza maisha katika mji wa Sar-e Pol Zahab, karibu na mpaka wa Iraq.

Timu za uokoaji zilifanya kazi siku nzima ili kupata waathirika na kutoa msaada kwa wakazi wa mji huo.

Majengo yaliyojengwa hivi karibuni yahakupata hasara kubwa, lakini nyumba za zamani zimeharibiwa sana, hasa katika maeneo ya vijijini.

Maelfu ya mahema na mablanketi pamoja na mchele, chakula na maji safi vilisambazwa kwa wakazi wa Sar-e Pol Zahab, ambao watalala nje kwa usiku wa pili mfululizo.

Katika jiji la Sar-e Pol Zahab, hospitali kuu na nusu ya shule ziliharibiwa na hakuna huduma yoyote inayotolewa katika.

Zaidi ya vijiji mia moja viliharibiwa na tetemeko hilo la ardhi.

Mamia ya watu waliojeruhiwa walihamishwa na kupelekwa kwenye hospitali za mikoa jirani na hata katika hospitali za mjini Tehran.

Serikali na vikosi vya jeshi, ikiwa ni pamoja na kikosi cha ulinzi wa Mapinduzi, kikosi maalumu cha jeshi, walitumia njia zote ili kuleta misaada kwa manusura.

Kwa mujibu wa viongozi, shughuli za uokoaji zimemalizika. Changamoto sasa ni kuwapa hifadhi maelfu ya watu wakati ambapo majira ya baridi yanakaribia.

Huduma za maji na umeme zimekatwa katika miji mingine na baada ya majengo kuporomoka watu walilazimika kulala nje kwenye baridi.

Shirika moja la utoaji misaada lilisema kuwa watu 70,000 wanahitaji makao baada ya tetemeko hilo, na kuna ripoti kuwa maelfu ya watu huenda wakalala nje kwa usuku wa pili.

Maafisa nchini Iran wanasema kuwa watu 413 wameuawa nchi humo. Baadhi ya wanajeshi na walinzi wa mpaka ni kati ya wale waliouawa.

Nchini Iraq watu 9 waliuawa kwa mujibu wa msemaji wa shirika la msalaba mwekundu. Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini humo ilisema kuwa watu 500 walijeruhiwa huko na tetemeko hilo lilisikika huko Irbil, Sulaimaniya, Kirkuk, Basra na mji mku Baghdad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.