Pata taarifa kuu
IRAQ-IS

Fallujah yakombolewa kutoka mikononi mwa IS

vikosi vya Iraq vimesema Jumapili hii kwamba vimeukomboa mkoa wote wa Fallujah baada ya operesheni ya zaidi ya mwezi mmoja na Waziri Mkuu ameweka muda wa mwisho kwa mkoa wa Mosul kuwa tayari kukombolewa. Mosul, ni ngome ya mwisho ya kundi la Islamic State kundi (IS) nchini Iraq.

Vikosi vya Iraq karibu na kijiji cha Falahat, magharibi mwa Fallujah.
Vikosi vya Iraq karibu na kijiji cha Falahat, magharibi mwa Fallujah. MOADH AL-DULAIMI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mbele ya hospitali ya mji, akivalia bendera shingoni mwake, Waziri Mkuu Haider al-Abadi amewataka "raia wa Iraq popote pale walipo kujitokeza kwa wingi mitaani na kusherehekea" kukombolewa kwa mkoa wa Fallujah, ngome ya wanajihadi, kilomita 50 magharibi mwa mji mkuu wa Iraq, Baghdad, akizungumza kuwa huu ni wakati wa "furaha".

"Tutapandisha bendera ya nchi ya Iraq hivi karibuni katika mkoa wa Mosul," Haidar al-Abadi aliongeza akimaanisha mji wa pili kwa ukubwa, uliyoko kaskazini.

Falluja ulikuwa mji wa kwanza nchini Iraq kuanguka mikononi mwa kundi la Islamic State mwezi Januari 2014. Wanajihadi kisha waliendesha mashambulizi makubwa yaliyowawezesha kulishinda jeshi la Iraq na kuyateka maeneo makubwa upande wa magharibi na kaskazini mwa mji mkuu Baghdad.

Lakini kwa zaidi ya mwaka, kundi la Islamic State imepoteza theluthi mbili ya maeneo hayo kufuatia kusonga mbele kwa majeshi ya Iraq yanayoungwa mkono na mashambulizi ya anga ya muungano wa kimataifa unaongozwa na Marekani.

Baada ya kuukomboa mji wa Ramadi, mji mkuu wa jimbo kubwa la magharibi la Al-Anbar, majeshi ya Iraq yalianzisha mashambulizi dhidi ya mkoa wa Fallujah Mei 23.

Vikosi vya Iraq hatimaye vilitangaza ushindi Jumapili baada ya kukiweka kwenye himaya yao kitongoji cha Al Jolan, ambapo lilikuwa lilikimbilia kundi la mwisho la wanajihadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.