Pata taarifa kuu
SYRIA-UTURUKI-IS-SHAMBULIZI

Roketi zarushwa kutoka Syria hadi Uturuki

Watu wawili, ikiwa ni pamoja na mvulana, wameuawa na wengine wawili wamejeruhiwa Jumanne hii katika mji wa Uturuki wa Kilis, ulio karibu na mpaka, katika mlipuko wa roketi 8 zilizorushwa kutoka nchini Syria, Meya wa Kilis na vyanzo vilio karibu na vyombo vya usalama wamebaini.

Juni 27, kwenye mpaka wa Uturuki na Syria, askari wa Uturuki akiangalia kwa mbali mji wa Kobane, Syria, ambako mapigano yanaendelea kati ya wapiganaji wa kundi la Islamic State na wapiganaji wa Kikurdi.
Juni 27, kwenye mpaka wa Uturuki na Syria, askari wa Uturuki akiangalia kwa mbali mji wa Kobane, Syria, ambako mapigano yanaendelea kati ya wapiganaji wa kundi la Islamic State na wapiganaji wa Kikurdi. AFP PHOTO/BULENT KILIC
Matangazo ya kibiashara

Meya wa mji wa Kilis, Hasan Kara, ameliambia shirika la habari la Uingereza la Reuters kwamab anafikiri ni shambulizi la makusudi kutoka eneo moja nchini Syria linalodhibitwa na wapiganaji wa kundi la Islamic State (IS).

Katika mji wa Izmir ambako Waziri Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu anakutana na mwenzake wa Ugiriki Alexis Tsipras, pia amelishtumu kundi la lslamic State kuhusika na urushaji wa roketi, ambazo zinaonyesha, kwa mujibu wa Waziri Mkuu wa Uturuki, jinsi gani hali bado ni tete nchini Syria.

Roketi moja imeanguka katika eneo lililo karibu na hospitali na nyingine katika eneo la makazi karibu na shule. Jeshi la Uturuki limejibu mashambulizi hayo, chanzo kilio karibu na vyombo vya usalama, kimesema.

Shule za mji wa Kilis zimefunga baada ya tukio hilo lakini hali ya utulivu imekua ikijiri katika mji huo, Meya wa mji wa Kilis amesema.

Meya wa mji wa Kilis akinukuliwa na kituo cha CNN-Turk, amesema roketi 8 zimeanguka katika eneo la makazi, karibu ya shule ya sekondari ya mji huo karibu na mpaka wa Syria, ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.