Pata taarifa kuu
URUSI-A-MASHAMBULIZI-USALAMA

Ndege za jeshi la Urusi zaanzisha mashambulizi Syria

Urusi imeendesha mashambulizi yake ya kwanza katika jimbo la Homs Jumatano asubuhi wiki hii. Operesheni hiyo imeendeshwa kwa ushirikiano na jeshi linalomuunga mkono Rais wa Syria Bashar Al Assad.

Ndege za kivita za Urusi MIG-29, katika kambi ya jeshi Machi 2015.
Ndege za kivita za Urusi MIG-29, katika kambi ya jeshi Machi 2015. AFP PHOTO / SERGEY VENYAVSKY
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hili, ambalo limethibitishwa na Urusi Jumatano hii mchana, linakuja baada ya kupitishwa mapema asubuhi, kwa neema za kuingilia kijeshi, hasa kwa mashambulizi ya anga. Leng ni kumsaidia Rais wa Syria Bashar Al Assad katika vita vyake “ dhidi ya ugaidi na msimamo mkali”.

Vikosi vya jeshi vya Urusi vilioko nchini Syria vimeendesha mashambulizi yao ya kwanza karibu na mji wa Homs, mji ambao unadhibitiwa kwa asilimia hamsini na waasi wa Syria. Wanajeshi wa Urusi waliotumwa nchini Syria kuunga mkono serikali ya Bashar al-Assad waaliionya Marekani, inayongoza muungano wa kimataifa unaoendesha mashambulizi nchini Syria kwa zaidi ya mwaka mmoja, kwa mujibu wa afisa wa ulinzi wa Marekani.

Operesheni pamoja na jeshi la Syria

Operesheni hiyo imeendeshwa " kulingana na uamuzi wa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi Vladimir Putin ", Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Urusi, jenerali Igor Konachenkov, ameelezea mashirika ya habari ya Urusi. " Ndege zetu zimetekeleza mashambulizi ya anga na yamefanya mashambulizi sahihi yaliyolenga ngome na maeneo yanayoshikiliwa na magaidi wa kundi la Islamic State nchini Syria ", ameongeza jenerali Konachenkov. Mashambulizi hayo yamelenga " vifaa vya kijeshi " na " ghala za silaha na risasi " za kundi la Islamic State (IS).

Operesheni imeendeshwa kwa ushirikiano na jeshi la Syria. Kwa mujibu wa chanzo katika Idara za usalama za Syria kiliyonukuliwa nashirika la habari la Ufaransa la AFP, "ndege za Urusi na Syriazimeendesha leo mashambulizi mengi dhidi ya ngome za magaidi katika miji ya Hama, Homs na Latakia."

" Njia pekee ya kupambana vilivyo dhidi ya ugaidi wa kimataifa nchini Syria nchi jirani, ni kufanya haraka, kwa kupambana na kuwaangamiza wapiganaji na magaidi katika maeneo wanayoshikiliana si kusubiri mpaka wao kuja kwetu ", amesema Rais wa Urusi Vladimir Putin katika hotuba iliyorushwa hewani kwenye televisheni dakika chache baada ya uthibitisho wamashambulizi hayo ya kwanza ya Urusi nchini Syria.

Lakini kwa mujibu wa Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Laurent Fabius, mashambulizi ya Urusi hayakulenga kundi la Islamic State.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.