Pata taarifa kuu
IRAQ-Kurdistan-IS-Siasa-Ushirikiano-Usalama

Haidar al-Abadi ajizolea sifa

Mgogoro wa mafuta kati ya Baghdad na viongozi wa Kurdistan umepatiwa ufumbuzi: Mgogoro huu ulidumu zaidi ya mwaka mmoja ambapo Baghdad na Erbil waliendelea kuzozana kuhusu usimamizi wa rasilimali za hydrocarbon kaskazini mwa Iraq.

Vikosi maalumu vya Iraq vikipambana, Juni 19 mwaka 2014.
Vikosi maalumu vya Iraq vikipambana, Juni 19 mwaka 2014. REUTERS/Stringer/Files
Matangazo ya kibiashara

Jumanne, Desemba 2, baada ya wiki kadhaa za mazungumzo, pande hizo mbili zilifikia mkataba, mkataba ambao unatazamia kutoa mamia kwa maelfu ya mapipa kwa siku kwa serikali ya Iraq sawa na kiwango kitakachotolewa kwa Kurdistan katika bajeti ya taifa. Mafanikio muhimu kwa waziri mkuu mpya, Haidar al-Abadi.

Hii pengine ni ushindi mkubwa wa kwanza wa kisiasa wa waziri mkuu mpya wa Iraq. Kwa mkataba huu, Haidar al-Abadi, amerejesha sehemu ya utajiri wa mafuta ambayo serikali yake hainufaiki nao. Aidha, mkutaba huu unaipunguzia Kurdistan wakati muhimu wa jitihada za kutetea uhuru wake. Mwisho lakini amefanikiwa pale ambapo al-Maliki alishindwa.

Chini ya miezi mitatu baada ya uteuzi wake, Haidar al-Abadi amefanikiwa zaidi kwenye wadhifa huo kuliko mtangulizi wake. Kiongozi mpya wa serikali ya Iraq pia ameonekana ni mtu mwenye ujasiri baada ya kuwatimua baadhi ya vigogo katika uongozi wa jeshi, na kuanzisha kampeni dhidi ya rushwa. Hatimaye kwenye uwanja wa vita, jeshi linaonekana kuwa na uwezo wa kutosha. Kwa vyovyote vile kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam haliwezi kupata ushindi kama ilivyokua mwezi Agosti.

Haidar al-Abadi bado ana kazi kubwa ya kuifanya ambayo ni muhimu kwa taifa la Iraq : maridhiano na watu kutoka jamii ya Wasuni walio wachache. Tangu alipoingia madarakani, Haidar al-Abadi amekua akikutana na viongozi wa jamii ya Wasunni ambao wamebaini kwamba walitengwa na Nouri Al Maliki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.