Pata taarifa kuu
ISRAELI-PALESTINA-HAMAS-Siasa-Usalama

Israeli : Gaza : idadi ya vifo yaendelea kuongezeka

Jitihada za kushawishi jeshi la Israeli na Hamas kusitisha mapigano zinaendelea, wakati mapigano hayo yameingia ijumaa wiki hii kwa siku ya 18, huku idadi ya vifo kutoka pande zote ikiendelea kuongezeka.

Mashambulizi ya jeshi la Isreali yaendelea katika ukanda wa Gaza kwa siku ya 18.
Mashambulizi ya jeshi la Isreali yaendelea katika ukanda wa Gaza kwa siku ya 18. REUTERS/Suhaib Salem
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi ya jeshi la Israeli katika ukanda wa Gaza yamesababisha vifo vya wapalestina 800, huku jeshi la Israeli likimpoteza leo ijumaa mwanajeshi wake mmoja na kutimiza idadi ya wanajeshi 33 wa Israeli ambao wameuawa katika mapigano hayo yanayoendelea.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon. ( Photo : Reuters )

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ametolea wito Israeli na Hamas kusitisha mapigano.

“Ninaambia Israeli na Hamas kwamba nafsi zao zitawasuta kuona wanaendelea kuua ndugu zao. Kwa hiyo muda umewadia wa kuweka silaha chini na kuketi kwenye meza ya mazungumzo kuliko kuuana”, amesema Ban.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Israeli, Baraza la Usalama la kitaifa la Israeli linatazamiwa kukutana ijumaa wiki hii mchana, ili kutafakari pendekezo la kusitisha mapigano liliyotolewa na waziri wa marekani mwenye dhamana ya mambo ya nje, John Kerry, ambaye amekutana kwa mazungumzo nchini Misri na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na mwenziye wa Misri Sameh Choukry.

Hamas kwa upande wake imeendelea kutoa masharti ya kuondolewa kwa vizuizi vya Israeli ili wapalestina waendeshe shughuli zao wakiwa huru.

Wakati hayo yakijiri, mfalme Abdallah wa Saudia Arabia, ameamuru msaada wa dola miloni 25.7 ili kusaidia sekta ya afya huko Palestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.