Pata taarifa kuu
UGANDA

Uganda: Bobi Wine azuiliwa tena kufanya kampeni

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine amezuiwa tena kuhutubia wafuasi wake.

Mgombea urais nchini Uganda, ambaye pia ni mwanamuziki, Bobi Wine.
Mgombea urais nchini Uganda, ambaye pia ni mwanamuziki, Bobi Wine. AFP Photos/ Guillem Sartorio
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano alikamatwa na polisi, pamoja na wajumbe kadhaa wa timu yake wakati wakifanya kampenikatika wilaya ya Kisiwa cha Bugala kaskazini mwa Ziwa Victoria.

Bobi Wine alikuwa ameanza tena kampeni yake ya urais nchini Uganda.

Mwanamuziki huyo ambayekwa sasa ni mmoja wa wanasiasa wakuu wa upinzani na mkosoaji mkuu wa rais Yoweri Museveni alirejeshwa nyumbani kwake huko Magere, katika mji mkuu Kampala, chini ya ulinzi mkali wa polisi.

Polisi wa Uganda wanalaumu mpinzani mkuu wa Yoweri Museveni kwa kukiuka sheria za kupambana na janga la COVID-19 na kukanusha kuwa wamemkamata.

"Mgombea huyo alishikiliwa kwa kuendelea kuandaa mikutano mikubwa wakati nchi inakabiliwa na tishio la janga la COVID-19, kwa kupuuza maagizo ya tume ya uchaguzi na Wizara ya Afya," polisi imesema katika .

Tukio hilo lilitokea katika wilaya ya Kalangala, kwenye Kisiwa cha Bugala kaskazini mwa Ziwa Victoria.

Hii sio moja ya maeneo ambayo kampeni imepigwa marufuku kwa sababu ya COVID-19.

Hii ilikuwa kwenye ajenda ya mzunguko wa kampeni yetu, "amesema msemaji wa chama cha Bobi Wine, Joel Ssenyonyi.

Bobi Wine ameibuka kuwa mshindani mkali wa Rais Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 76, kuelekea uchaguzi mkuu wa Januari 14.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.