Pata taarifa kuu
TANZANIA-CHADEMA-SIASA-USALAMA

Tundu Lissu: Ninaamua kurejea nchini Tanzania licha ya kuhofia usalama wangu

Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu  ambaye amekuwa akipata matibabu nchini Ubelgiji, baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana jijini Dodoma mwaka 2017 anatarajiwa kurejea nchini mwake leo Jumatatu, wakati huu polisi wakizuia mikusanyiko ya watu kwenda kumpokea.

Mwanasiasa mashuhuri wa upinzania Tanzania, Tundu Lissu akizungumza katika Hospitali ya Nairobi Januari, 2018
Mwanasiasa mashuhuri wa upinzania Tanzania, Tundu Lissu akizungumza katika Hospitali ya Nairobi Januari, 2018 The Citizen
Matangazo ya kibiashara

Tundu Lissu, ni wakili na mwanasiasa mwenye umri wa miaka 58, lakini pia  Naibu Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini humo  CHADEMA.

Amekuwa mkosoaji mkubwa wa rais John Magufuli, kusababisha kukamatwa kwake mara kadhaa.

Mwaka 2017, alikamatwa na maafisa wa usalama mara sita kwa kile kilichoelezwa ni kumkosea heshima rais Magufuli  kwa  kumwita Dikteta.

Mambo yalikuwa mabaya zaidi mwezi Septemba mwaka 2017 wakati wa kikao cha bunge jijini Dodoma, aliposhambuliwa na watu wasiojuliana na na kujeruhiwa vibaya.

Alipata majereha 18 katika mwili wake na kukimbizwa jijini Nairobi nchini Kenya kupata matibabu kabla ya kuhamishiwa nchini Ubelgiji kupata matibabu zaidi.

Baada ya mkasa huo, rais Magufuli kupitia ukurasa wake wa Twitter, aliandika kusikitishwa na kushambuliwa kwa Lissu, na kumtakia nafuu ya haraka.

Kushambuliwa kwa Lissu, kumeendelea kulaaniwa na watetezi wa haki za binadamu na viongozi wa dini nchini Tanzania, na ameamua kurejea nyumbani licha ya wito wa familia yake kumtaka asifanye hivyo.

Wakili wake ameindikia barua serikali ya Tanzania, kutaka mwanasiasa huyo kupewa ulinzi atakapowasili nchini humo.

Tundu Lissu, amechukua fomu ya kuomba tiketi ya kuwania urais kupitia chama chake cha CHADEMA wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka hu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.