Pata taarifa kuu
TANZANIA-SIASA-USALAMA

Serikali ya Tanzania yautaka upinzani kutoingilia masuala ya jinai

Siku chache baada ya mahakama ya hakimu mkazi nchini Tanzania kutoa hukumu ya kesi ya uchochezi iliyokuwa ikiwakabili wanasiasa wa upinzani, serikali ya nchi hiyo imewataka wanasiasa wa upinzani kuacha kufanya siasa kwenye masuala ya jinai.

Wafuasi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, wakiwa kwenye moja ya mikutano ya chama hicho wakati wa kampeni za urais mwaka jana.
Wafuasi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, wakiwa kwenye moja ya mikutano ya chama hicho wakati wa kampeni za urais mwaka jana. RFI
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya serikali ya Tanzania imetolewa na msemaji wa serikali Dr Hassan Abbas ambaye anasema serikali itaendelea kuchukua hatua dhidi ya mtu yeyote anayejihusisha na makosa ya jinai.

Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo, Chadema, na kiongozi wa upinzani katika bunge la Tanzania,

Freeman Mbowe, amesema licha ya changamoto za kisiasa, chama chake kitaendelea kupigania haki katika taifa.

Wafuasi wa chama cha Chadema wameonesha uungwaji wao mkono kwa kiongozi wa chama hicho, wakibaini kwamba upinzani nchini Tanzania, hasa chama chao kinanyanyaswa na vyombo vya dola.

Siku kadhaa zilizopita Rais wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli aliihakikishia Jumuiya ya kimataifa kuwa Uchaguzi mkuu nchini humo uliopangwa kufanyika Oktoba mwaka huu utakuwa huru na wa haki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.