Pata taarifa kuu
BURUNDI-CNL-UCHGUZI-SIASA-HAKI

Uchaguzi Burundi: Chama cha CNL chawasilisha malalamiko yake mbele ya Mahakama ya Katiba

Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Burundi, CNL, Agathon Rwassa amewasalisha kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika hivi karibuni.

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha CNL, Agathon Rwasa.
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha CNL, Agathon Rwasa. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Tume ya uchaguzi nchini humo,CENI ilimtangaza Evariste Ndayishimiye mshindi wa kura hizo japo upinzani na Kanisa Katoliki kutilia shaka matokeo hayo yakidai kuwepo na udanganyifu mkubwa wa kura.

Katikati mwa wiki hii Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Burundi walisema, Uchaguzi Mkuu uliofanyika wiki iliyopita, uligubikwa na udanganyiku mkubwa na hivyo wanatilia shaka ushindi wa mgombea wa chama tawala, Evariste Ndayishimiye aliyetangazwa mshindi na Tume ya Uchaguzi wiki hii.

Chama cha CNL kimesema kuwa kina ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumatano Mei 20 uligubikwa na wizi wa kura.

Chama hicho kimesema kina imani na Mahakama ya Katiba kwamba itakitendea haki, la sivyo kitawasilisha malalamiko yake mbele ya mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu.

Tume Huru ya Uchaguzi nchini Burundi, CENI, ilimtangaza Jenerali Evariste Ndayishimiye mshindi katika uchaguzi wa urais uliofanyika Jumatano Mei 20, 2020 kwa kupata 68.72% ya kura dhidi ya mshindani wake mkuu Agathon Rwasa aliyepata 24.19% ya kura.

Iwapo Mahakama ya Katiba itahibitisha matokeo ya uchaguzi Jenerali Evariste Ndayishimiye atakuwa rais wa tatu aliyechaguliwa chini ya misingi ya kidemokrasia tangu nchi hiyo kupata uhuru wake Julai 1, 1962, na hivyo kuchukuwa mikoba ya mtangulizi wake Pierre Nkurunziza kutoka chama cha CNDD-FDD.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.