Pata taarifa kuu
BURUNDI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Evariste Ndayishimiye atangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais Burundi

Tume Huru ya Uchaguzi nchini Burundi, CENI imemtangaza mgombea wa chama tawala cha CNDD-FDD Jenerali Evariste Ndayishimiye kuwa ameshinda uchaguzi wa urais uliofanyika Jumatano wiki iliyopita nchini humo.

Jenerali Evariste Ndayishimiye amepata asilimia 68.72 za kura.
Jenerali Evariste Ndayishimiye amepata asilimia 68.72 za kura. STRINGER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Awali Agathon Rsawa alitangaza kwamba hatakubaliana na matokeo ya uchaguzi , akibaini kwamba Uchaguzi Mkuu uliofanyika juma lililopita uligubikwa na udanganyifu mkubwa, kura nyingi zilibwa upande wa chama chake.

Hata hivyo Tume Huru ya Uchaguzi Ceni imesema yoyote ytule ambaye hatakubaliana na matokeo ana fursa yakutoa malalamiko yake mbele ya Mahakama ya Katiba kwa muda maalumu.

Kulingana na matokeo hayo ya uchaguzi yaliyotangazwa na CENI, chama tawala cha CNDD-FDD kimeshinda viti 72 katika Bunge la Seneti, chama cha CNL viti 27 na chama cha Uprona cha makamu wa kwanza wa rais anaye maliza muda wake Gaston Sindimwo kimepata kiti kimoja.

Jenerali Evariste Ndayishimiye anakuwa rais wa tatu kuchaguliwa katika misingi ya kidemokrasia baada ya mtangulkizi wake Pierre Nkurunziza (2005, 2010, 2015) na Melchior Ndadaye ( mwaka 1993).

Evariste Ndayioshimiye anadsubiri kuthibitishwa na Mahakama ya Katiba na hivyo kuwa rais rasmi wa taifa la Burundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.