Pata taarifa kuu
BURUNDI-NDAYISHIMIYE-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Mfahamu rais mteule wa Burundi Jenerali Evariste Ndayishimiye

Tume Huru ya Uchaguzi nchini Burundi, CENI imemtangaza mgombea wa chama tawala cha CNDD-FDD Jenerali Evariste Ndayishimiye kuwa ameshinda uchaguzi wa urais uliofanyika Jumatano wiki iliyopita nchini humo kwa kura 68.72 dhidi ya 24.19 alizopata mshindani wake mkubwa Agathon Rwasa.

Evariste Ndayishimiye, hapa na mkewe Angelique Ndayubaha, katika kituo cha kupigia kura katika eneo la Giheta, katika mkoa wa Gitega, katikati mwa Burundi, siku ya uchaguzi, Mei 20, 2020.
Evariste Ndayishimiye, hapa na mkewe Angelique Ndayubaha, katika kituo cha kupigia kura katika eneo la Giheta, katika mkoa wa Gitega, katikati mwa Burundi, siku ya uchaguzi, Mei 20, 2020. AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Chama kikuu cha upinzani nchini Burundi CNL kupitia msemaji wake Therence Manirambona, kimekataa kutambua ushindi wa Evariste Ndayishimiye wa chama tawala CNDD FDD kama mshindi wa Uchaguzi wa urais uliofanyika wiki iliyopita.

Evariste Ndayishimiye anasubiri matokeo hayo yathibitishwe na Mahakama ya Katiba ili achukuwe hatamu ya uongozi wa nchi.

Hata hivyo Afisaa huyo wa juu wa zamani wa jeshi la Burundi kutoka kundi la zamani la waasi la CNDD-FDD anasubiriwa na kibaruwa kikubwa katika kuendeleza gurudumu la taifa hilo ndogo Afrika Mashariki na Kati.

Jenerali Evariste Ndayishimiye, alipeperusha bendera ya chama tawala CNDD-FDD hadi kukifikisha kwenye ushindi wakati wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumatano Mei 20, 2020 na ni Katibu mkuu wa chama hicho ambacho kimekuwa madarakani kwa miaka 15 baada ya kutia saini kwenye mkataba wa amani wa Arusha mwaka 2000.

Ndayishimiye, ana umri wa miaka 52, mwanajeshi wa muda mrefu nchini Burundi na anafahamika kwa jina maarufu la Neva.

Mwezi Januari, baada ya kuomba kustaafu katika jeshi, aliteuliwa na chama chake kuwania urais na kuchukuwa mikoba ya rais Pierre Nkurunziza, ambaye alikuwa ametangaza kuwania hatowania tena wadhifa huo.

Wanaomfahamu wanasema yeye ni mtu msikivu, lakini mwenye msimamo mkali na hajahusishwa na visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyodaiwa kutekelezwa na baadhi ya vigogo wa chama hicho kwa mujibu wa mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Ripoti zinasema kuwa Nkurunziza alimtaka spika wa Bunge Pascal Nyabenda, kumrithi lakini Majenerali wa kijeshi wakaamua kuwa Jenerali mwenzao Ndayishimiye, ambaye alishiriki katika vita dhidi ya serikali wakati huo wakiwa waasi wa Kihutu, apewe nafasi hiyo.

Mmoja wa viongozi wa chama cha CNDD-FDD ambaye hakutaka jina lake litajwe alinukuliwa na shirika la Habari la AFP akisema kuwa Ndayishimiye ni mwaminifu na yupo tayari kukifia chama.

Wadadisi wa siasa nchini humo wanahoji iwap atasimamia mambo anayoyaamini au atatumiwa na viongozi wa zamani kulinda maslahi yao? Tusubiri tuone.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.