Pata taarifa kuu
BURUNDI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Matokeo ya awali ya Uchaguzi Mkuu kutangazwa Burundi

Tume Huru ya Uchaguzi nchini Burundi (CENI) hii leo Jumatatu alaasiri itatangaza matokeo ya awali ya uchaguzi uliofanyika Jumatano ya juma lililopita, huku kukiwa na taarifa kwamba matokeo ya awali yanaonyesha mgombea wa chama tawala, Évariste Ndayishimiye, anaongoza.

Chama kikuu cha upinzani cha CNL cha Agathon Rwasa kimebaini kwamba Uchaguzi Mkuu wa Mei 20 uligubikwa na udangayifu mkubwa.
Chama kikuu cha upinzani cha CNL cha Agathon Rwasa kimebaini kwamba Uchaguzi Mkuu wa Mei 20 uligubikwa na udangayifu mkubwa. REUTERS/Paulo Nunes dos Santos
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa yake kwa vyombo vya habari Jumapili Mei 24, Tume Huru ya Uchaguzi nchini Burundi imefahamisha kuwa matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais, wa wabunge na serikali za mitaa uliofanyika Jumatano Mei 20 yatatolewa hii leo Jumatatu kuanzia zaa nane alaasiri kwa saa za Bujumbura, huku matokeo ya mwisho yakisubiriwa hadi Juni 4 mwaka huu.

Matokeo ya awali yanaonyesha kuwa mgombea wa chama tawala CNDD-FDD, Jenerali Evariste Ndayishimimye, mwenye umri wa miaka 52, anaongoza kwa uwingi wa kura, jambo ambalo mgombea wa chama cha upinzani Agathon Rwasa ametupilia mbali, huku akisisitiza kuwa chama chake cha CNL kinaongoza katika chaguzi zote zilizofanyika.

Rwasa amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa kwake yeye hakuna swali la kujadili chochote, uchaguzi wa watu lazima uheshimiwe.

Evariste Ndayishimiye ameonekana kumrithi rais anayemaliza muhula wake wa tatu Pierre Nkurunziza, aliyeingia madarakani tangu mwaka 2005, ambapo mwaka 2015 upinzani ulipinga muhula wake wa tatu na kusababisha nchi hiyo kuingia katika machafuko ya baada ya uchaguzi, na hali ya sintofahamu ya kisiasa kuligubika taifa hilo ndogo la Afrika ya kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.