Pata taarifa kuu
BURUNDI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Uchaguzi Burundi: Kiongozi wa upinzani afutilia mbali matokeo ya awali

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzaji nchini Burundi, Agathon Rwasa, ameelezea matokeo ya awali yanayompa ushindi mkubwa mgombea wa chama tawala cha CNDD-FDD Evariste Ndayishimiye kama "kichekesho".

Zoezi la kupiga kura huko Gitega, Burundi, Mei 20, 2020.
Zoezi la kupiga kura huko Gitega, Burundi, Mei 20, 2020. REUTERS/Evrard Ngendakumana
Matangazo ya kibiashara

Matokeo hayo ambayo yalitangazwa Alhamisi jioni wiki hii kwenye Redio na Televisheni vya taifa yanahusu kura zilizohesabiwa katika 12% ya tarafa 119 za Burundi.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi (CENI), Pierre-Claver Kazihise alikuwa amewatolea wito wananchi wa Burundi siku ya Alhamisi asubuhi kuwa na subira kwa kusubiri matokeo ya awali kutangazwa leo Ijumaa Mei 22 .

"Ninafutilia mbali matokeo haya. Matokeo haya ambayo wako watangaza ni matokeo bandia, hayaendani na ukweli," Rwasa amesema Alhamisi jioni.

"Ninasema hivyo kwa sababu jana (Jumatano jioni) wakati tulianza kuhesabu kura, tulifuata taarifa kutoka vituo mbalimbali vya kupigia kura, tulikuwa tunakaribiana kwa kura na matokeo ambayo tunayo sasa ni kuwa bado tunaongoza", ameongeza.

"Tunaweza kuonyesha kwa urahisi kuwa ni wizi wa kura" Agathon Rwasa amebaini, huku akidai kuwa "ameshinda".

"Takwimu zinazotolewa kupitia Redio na televisheni vya taifa ni matokeo ya ujanja tu", amesema.

Matokeo haya ya awali yanampa mgombea wa chama tawala cha CNDD-FDD Evariste Ndayishimiye ushindi wa 73.9% ya kura dhidi ya 24.6% alizopata Bw. Rwasa katika wilaya ya Kabezi, mkoani Bujumbura, ambayo ngome ya kihistoria ya kiongozi wa wa chama cha upinzani cha CNL.

Chaguzi hizi, ambazo kwa ujumla zilifanyika kwa utulivu, zinaashiria mwisho wa utawala wa Nkurunziza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.