Pata taarifa kuu
BURUNDI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Mfahamu mgombea wa chama kikuu cha upinzani cha CNL Agathon Rwasa

Agathon Rwassa, mgombea wa urais kupitia chama kikuu cha upinzani cha CNL, anatarajiwa kuleta upinzani mkali katika uchaguzi huu, na ni kwa mara ya kwanza anawania kwenye kiti cha urais tangu alipojiunga na warundi wenzake katika mchakato wa Amani baada ya kusaini mkataba wa amani mwaka 2006.

Agathon Rwasa, mmoja wa wapinzani wakuu nchini Burundi, kiongozi wa chama cha CNL, mgombea urais wa mwaka 2020, kwenye kampeni yake ya uchaguzi.
Agathon Rwasa, mmoja wa wapinzani wakuu nchini Burundi, kiongozi wa chama cha CNL, mgombea urais wa mwaka 2020, kwenye kampeni yake ya uchaguzi. © CNL, Inyankamugayo
Matangazo ya kibiashara

Kabla ya kuingia kwenye ulingo wa kisiasa, Rwasa mwenye umri wa miaka 56, alikuwa kiogozi wa kundi la waasi la Kihutu la FNL mapema miaka ya 2000 na kundi lake kutuhumiwa kuwatumia watoto katika jeshi lake.

Baada ya vita vya zaidi ya miaka 20 alirudi nyumbani mwaka 2008, lakini kabla ya hilo, kundi lake la FNL lilitia saini mkataba wa amani na serikali mwaka 2006.

Mwaka 2010, alitanagza kujificha baada ya kudai kuwa serikali ya Bujumbura ilikuwa inapanga kumkamata kwa kuwa na mpango wa kuyumbisha usalama wa taiafa na mwaka uho huo akaondolewa katika uongozi wa chama cha FNL,  na baadaye akaamua kuunda muungano wa kisiasa unaofahamika kama Amizero y' Abarundi lakini akasusia kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka 2015 kwa madai kuwa haungekuwa huru na haki lakini pia alichaguliwa kuwa naibu spika wa bunge.

Baada ya marekebisho ya Katiba mwaka 2018, Rwasa aliunda chama kipya cha CNL na kuwa chama kikuu cha upinzani nchini humo na mwezi Februari aliteuliwa na chama chake kuwania urais.

Mwanasiasa huyo amekuwa akisema kuwa ana matumaini ya kupata ushindi na kumrithi rais Nkurunziza iwapo uchaguzi utakuwa huru na haki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.