Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-KIIR-MACHAR

Waasi nchini Sudan Kusini wapinga mapendekezo ya rais Kiir kuhusu idadi ya majimbo

Waasi nchini Sudan Kusini wamekataa pendekezo la rais Salva Kiir kuwa, nchi hiyo irejee kwenye mfumo wa kuwa na majimbo 10, kama njia mojawapo ya kumaliza mzozo ambao umekuwa ukiendelea kwa miaka sita sasa na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 380,000.

Kiongozi wa upinzani nchini Sudan Riek Machar
Kiongozi wa upinzani nchini Sudan Riek Machar © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Rais Kiir amesema kwa upande wake, yupo tayari kupunguza idadi ya majimbo kutoka 32 hadi 10 kama ambavyo waasi walikuwa wanadai hapo awali, ili pande zote mbili zifanikiwe kuunda serikali ya pamoja hivi karibuni.

Hata hivyo, pamoja na kusema kuwa yupo tayari kupunguza idadi hiyo, Kiir  amesema serikali ya Juba itasimamamia majimbo ya Pibor, Ruweng na Abyei.

Hatua hiyo imemkera kiongozi wa waasi Riek Machar ambaye amesema mapendekezo ya rais Kiir, hayakubaliki kwa kile alichosema kuwa yatasababisha matatizo zaidi.

Kiir na Machar, wanaendelea kupata shinikizo za Kimataifa kukubaliana ili kuunda serikali hiyo ya pamoja kufikia tarehe 22, ili kuanza kutekelezwa kwa kikamilifu mkataba wa amani wa mwaka 2018.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.