Pata taarifa kuu
TANZANIA-HRW-HAKI-USALAMA

HRW yaituhumu Tanzania kuminya haki za afya za wapenzi wa jinsia moja

Shirika la Kimatafa la Haki za Binaadamu la Human Rights Watch limeinyooshea kidole cha lawama serikali ya Tanzania kwa kuminya haki za afya za wapenzi wa jinsia moja kwa kuwazuia kupata huduma na haki za msingi za kisheria na haki zingine za binadamu.

Mji wa Dar es Salaam. Mwezi Novemba 2018, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda alitoa wito kwa wakazi wa mji huo "kuwataja wapenzi wa jinsia moja na kuwafikisha mbele ya vyombo vya usalama".
Mji wa Dar es Salaam. Mwezi Novemba 2018, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda alitoa wito kwa wakazi wa mji huo "kuwataja wapenzi wa jinsia moja na kuwafikisha mbele ya vyombo vya usalama". Wikimédia/Muhammad Mahdi Karim
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti yake, shirika hilolinasema wamekusanya ushahidi unaoelezea namna gani haki za wapenzi wa jinsia moja zimekuwa zikikiukwa, hususan kunyimwa huduma za afya, kulazimisha kufanya vipimo vya njia ya haja kubwa.

Mwezi Novemba 2018, Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda alitoa wito kwa wakazi wa mji huo "kuwataja wapenzi wa jinsia moja na kuwafikisha mbele ya vyombo vya usalama".

Mwaka 2016 serikali ya Tanzania kupitia wizara ya afya ilipiga marufuku mashirika ya kiraia kusambaza vilaini bure kwa wanaume wanaovutiwa kimapenzi na wanaume wenzao kama sehemu ya jitihada za kupambana na maambukizi ya UKIMWI.

Katika miaka ya hivi karibuni, operesheni ya kamata kamata dhidi ya jamii ya wapenzi wa jinsi moja imekuwa ikiendelea nchini Tanzania. Makonda, mshirika wa karibu wa Rais John Magufuli, na mwenye imani ya Kikristo, aliwataka wananchi wenzake kuunga mkono kampeni yake dhidi ya ushoga, ambao, amesema, "umepoteza maadili ya Watanzania na dini zetu zote mbili Ukristo na Uislamu."

Wapenzi wa jinsia moja nchini Tanzania wameendelea kuishi kwa hofu, huku baadhi yao wakilazimika kuishi kwa kujificha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.