Pata taarifa kuu
RWANDA-UGANDA-USHIRIKIANO

Rwanda na Uganda kuhakikisha uhusiano kati yao umeimarika

Rwanda na Uganda zinasema zina dhamira ya dhati ya kutekeleza kikamilifu mkataba uliotiwa saini kati ya viongozi wa nchi hizo mbili mwezi Agosti jijini Luanda nchini Angola.

Rais wa Angola Joao Lourenço amezungukwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni (kushoto) na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame (kulia) baada ya kusaini makubaliano ya kumaliza uhasama, Agosti 21, 2019.
Rais wa Angola Joao Lourenço amezungukwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni (kushoto) na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame (kulia) baada ya kusaini makubaliano ya kumaliza uhasama, Agosti 21, 2019. JOAO DE FATIMA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kamati inayoshughulikia utekelezwaji wa mkataba huo ulikutaja jana jijini Kigali na miongoni mwa mambo mengine, wawakilishi wa nchi hizo mbili walikubaliana kukutana tena baada ya skiku 30 kuthathmini utekelezwaji wa mkataba huo.

Katika mkutano huo, Rwanda ilitoa majina ya raia wake inayoamini wanashikiliwa kinyume cha sheria nchini Uganda, hatua inayokuja baada ya Uganda wiki iloiyopita kuwaachilia huru raia wa Rwanda zaidi ya 30 kuelekea mkutano huo.

Agosti 21 mwezi uliopita, Marais Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda walisaini makubaliano ya amani katika mji mkuu wa Angola, Luanda yenye lengo la kumaliza uhasama na mzozo uliopo kati ya mataifa hayo mawili jirani.

Marais wa Rwanda na Uganda, Paul Kagame na Yoweri Museveni, 2018 Entebbbe.
Marais wa Rwanda na Uganda, Paul Kagame na Yoweri Museveni, 2018 Entebbbe. Michele Sibiloni / AFP

Marais hao walifikia makubaliano hayo katika mkutano wa pili huko Luanda mbele ya marais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Angola na Congo Brazaville waliokuwa wapatanishi katika mgogoro huo.

Joto la mzozo baina ya Rwanda na Uganda limekuwepo tangu mwanzoni mwa mwaka huu na limeathiri maisha ya watu kijamii na kiuchumi katika mataifa hayo jirani.

Maafisa nchini Rwanda wamekuwa wakiituhumu Uganda kwa kuwafunga na kuwatesa kinyume cha sheria raia wake nchini Uganda, wakati Uganda nayo inaituhumu Rwanda kutekeleza ujasusi katika ardhi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.