Pata taarifa kuu
RWANDA-UGANDA-USHIRIKIANO

Rwanda yafunga tena mpaka wake na Uganda

Serikali ya Rwanda imeunga tena mpaka wake na Uganda wa Katuna. Hatua hii inakuja, baada ya serikali ya Rwanda hapo awali, kukubali kufungua mpaka huo kwa muda wa siku 12 ili kuruhusu malori yenye mizigo yaliyokuwa yamekwama kupita.

Rais Kagame alisisitiza kwamba mara kadhaa mwenyewe aliwasilisha malalamiko hayo kwa mwenzake Yoweri Museveni na kwamba hakuonyesha utashi wowote wa kuyatatua.
Rais Kagame alisisitiza kwamba mara kadhaa mwenyewe aliwasilisha malalamiko hayo kwa mwenzake Yoweri Museveni na kwamba hakuonyesha utashi wowote wa kuyatatua. Fabrice COFFRINI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ilionekana kuwa hatua hiyo ya Kigali, ingemaliza uhusiano mbaya na serikali ya Kampala, ambao umekuwa ukishuhudiwa tangu mwezi Februari.

Nchi za Rwanda na Uganda zinashuhudia mvutano wa kidiplomasia. Rwanda inaishutumu Uganda kwa kuwaficha maadui wa serikali yake, suala ambalo Uganda inakanusha vikali.

Hivi karibuni Rais wa Rwanda Paul Kagame alielezea kuwa chimbuko la mgogoro baina ya nchi yake na nchi ya Uganda ni la tangu miaka 20 iliyopita, akilaumu nchi ya Uganda kutaka kuangusha utawala wake.

Rais Kagame alisema mgogoro huo ulishika kasi mnamo miaka ya hivi karibuni kutokana na serikali ya Uganda kuunga mkono kundi la RNC linalopinga utawala wa Kagame na ambalo linatumiwa na Uganda kuwanyanyasa raia wa Rwanda wanaotembelea au wanaoishi nchini Uganda.

“RNC wanafanya kazi kwa ushirikiano na vyombo vya usalama vya Uganda.kilicho wazi ni kwamba Wanachokifanya ni kunyanyasa wanyarwanda ambao hawataki kuungana nao huku wakiwasingizia a kwamba wametumwa na utawala wa Kigali kuhujumu usalama wa Uganda na kuuwa wanyarwanda wa upinzani.Ni madai yasiyo na msingi.lakini haya yote yanaonyesha ushirikiano wa dhati uliyopo baina ya serikali ya Uganda na kundi la RNC, '' rais Kagame alisema.

Rais Kagame alisisitiza kwamba mara kadhaa mwenyewe aliwasilisha malalamiko hayo kwa mwenzake Yoweri Museveni na kwamba hakuonyesha utashi wowote wa kuyatatua.

Hata hivyo Uganda imekuwa ikiishutumu Rwanda kuwatuma majasusi na kufanyia vitendo vya ujasusi kwenye ardhi yake,shutuma ambazo Rwanda inakanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.