Pata taarifa kuu
UGANDA-MALARIA-AFYA

Idadi ya wagonjwa wa Malaria yaongezeka Uganda

Wizara ya Afya ya Uganda, mapema wiki hii imetangaza kuongezeka kwa kesi za ugonjwa wa malaria nchini humo. Mamlaka nchini humo imeripoti kesi milioni 1.4 kati ya mwezi Juni na Agosti, sawa na asilimia 40, idadi kubwa zaidi ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Idadi ya kesi za ugonjwa wa malaria imeongezeka hadi 60% nchini Uganda ikilinganishwa na mwaka 2018.
Idadi ya kesi za ugonjwa wa malaria imeongezeka hadi 60% nchini Uganda ikilinganishwa na mwaka 2018. ESTHER MABABZI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Joto limekuwa kwenye kiwango cha juu na ugonjwa wa Malaria unaendelea kushika kasi katika maeneo mbalimbali nchini.

Mikoa ya kaskazini mwa nchi ndio imeathirika hasa. Lakini miji ambayo ilikuwa na kiwango cha chini sana cha ugonjwa wa malaria pia imeathirika. Katika mji wa Kampala, kwa mfano, ambapo kawaida hurupitiwa wagonjwa wa Malaria wasiozidi 1% , idadi ya wagonjwa imeongezeka kwa kiwango kikubwa, na kufikia 60% ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Idadi ya vifo, kwa upande mwingine, inaendelea kuongozeka. Ugonjwa wa Malaria umeua watu 1,600 tangu mwanzoni mwa mwaka huu nchini Uganda. Uganda sio nchi pekee inayoathirika na ugonjwa huo. Burundi pia inakabiliwa na mlipuko wa ugonjwa huo, ambapo karibu mtu mmoja kati ya watu wawili anaugua Malaria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.