Pata taarifa kuu
KENYA-USALAMA-UGAIDI

Idadi ya waliouawa katika shambulio Kenya yaongezeka na kufikia 21

Idadi ya watu waliouawa katika shambulio la wanamgambo wa Al Shabab kutoka Somalia dhidi ya hoteli ya kifahari ya DusitD2 jijini Narobi nchini Kenya, imeongezeka na kufikia 21, kwa mujibu wa vyanzo vya polisi.

Vikosi vya Usalama vikizingira hoteli ya kifahari iliyokuwa imevamia na kushambuliwa na wanamgambo wa Al Shabab, Nairobi, Kenya, Januari 15, 2019.
Vikosi vya Usalama vikizingira hoteli ya kifahari iliyokuwa imevamia na kushambuliwa na wanamgambo wa Al Shabab, Nairobi, Kenya, Januari 15, 2019. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Idadi hiyo mpya imetolewa saa chache baada ya Rais UhuruKEnyatta Juana Jumatano Jioni kutangaza kwamba watu waliopoteza maisha katika tukio hilo ni 14 lakini idadi ya wengine isiyojulikana wamejeruhiwa.

“Kwa sasa tunathibitisha kuwa watu waliopoteza maisha mikononi mwa magaidi ni 14, lakini wengine wamejeruhiwa,” alisema Rais Kenyatta.

Aidha, alibaini kwamba maafisa wa polisi na wasamaria wema walifanikiwa kuwaokoa watu 700.

Hata hivyo, haijafahamika magaidi waliotekeleza shambulizi hilo walikuwa wangapi lakini kamera za cctv zimeonesha watu wanne wakiwa na silaha wakiingia katika eneo la hoteli hiyo.

Polisi wamethibitisha kuwa, washambuliaji wawili waliuawa katika makabiliano makali ya risasi.

Kundi la Al Shabab kutoka nchini Somalia lilikiri kuwa limehusika na shambulio hilo.

Shambulizi hili, limewakumbusha wengi shambulizi la kigaidi lilitokea mwaka 2013 katika jengo la biashara la Westgate na kusababisha vifo vya watu 67.

Mwezi Aprili mwaka 2015 shambulizi lingine la kigaidi lilitokea katika Chuo Kikuu cha Garissa Mashariki mwa nchi hiyo na kusababisha vifo vya watu 148, wengi wao wakiwa wanafunzi.

Kenya ilianza kushuhudia milipuko ya kigaidi kutoka kwa kundi la Al Shabab mwaka 2011, baada ya kuwatuma wanajeshi wake nchini Somalia, kupambana na kundi hilo la kigaidi ambalo linapambana na serikali ya Mogadishu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.