Pata taarifa kuu
BURUNDI-EAC-USALAMA-SIASA

Museveni amtaka rais wa Burundi kuzungumza na wapinzani wake

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametoa wito kwa mwenzake wa Burundi Pierre Nkurunziza kuheshimu Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), mpatanishi katika mgogoro unaondelea kuikabili nchi yake, na kuzungumza na upinzani ulio nje ya nchi.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza na Rais wa Uganda Yoweri Museveni  Bujumbura tarehe 14 Julai 2015.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza na Rais wa Uganda Yoweri Museveni Bujumbura tarehe 14 Julai 2015. RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Rais Museveni amesema hayo katika barua ya hivi karibuni aliomuandika rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, barua ambayo imendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Katika barua hiyo ya Jumamosi tarehe 8 Desemba 2018 na ambayo uhalali wake umethibitishwa siku ya Alhamisi na ofisi ya rais wa Burundi, Rais Museveni, mpatanishi mkuu katika mgogoro wa Burundi kwa niaba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) amemkumbusha Nkurunziza kama jumuiya hiyo ya kikanda imechangia kwa kiasi kikubwa kwa kupatikana Mkataba wa amani Arusha wa mwaka 2000.

Mkataba huo muhimu ulipelekea kusitishwa kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Burundi ambapo watu zaidi ya 300,000 waliuawa kati ya mwaka 1993 na 2006), na kuanzisha mfumo wa kugawana madaraka kati ya makabila mawili makuu, Wahutu na Watutsi.

Rais wa Uganda, katika barua yake ambayo ni jibu kwa barua kutoka kwa mwenzake Nkurunziza ya tarehe 4 Desemba, amekwenda mbali hadi kusema kuwa kuna uwezekano Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) "kutumiwa" na Burundi.

Mvutano huu umeibuka baada ya Burundi kususia mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwishoni mwa mwezi Novemba. Mkutano ambao ulikuwa na lengo la kujadili kuhusu mgogoro wa Burundi, kabla ya siku chache baadaye Serikali ya Burundii kutaka mkutano huo ujadili tu "uhasama uliopo kati ya Rwanda".

Uhusiano kati ya nchi hizi mbili umedorora. Serikali ya Bujumbura inaishtumu Rwanda kuchochea machafuko nchini Burundi, tuhuma ambazo Rwanda inakanusha na kusema ni mpango wa serikali ya Bujumbura kutaka kuleta mgawanyiko.

Mkutano mpya wa viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umepangwa kufanyika Desemba 27, lakini haijulikani kama Bujumbura itashiriki mkutano huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.