Pata taarifa kuu
ALGERIA-AFRIKA MASHARIKI-SAYANSI-UTAFITI

Afrika Mashariki yaweza kupoteza sifa yake ya kipekee kama Chimbuko la binadamu

Wanaakiolojia wamegundua nchini Algeria masalia ya kale ya zana zilizotengenezwa kwa mawe tangu miaka milioni 2.4 iliyopita, masalia ya kale kuliko yale yaliyopatikana katika eneo la Afrika Mashariki hadi sasa.

Uvumbuzi ulifanyika kwenye maeneo mawili ya akiolojia, moja ya tangu miaka milioni 2.4 iliyopita na ya pili ya tangu miaka milioni 1.9 (Picha ya kumbukumbu)
Uvumbuzi ulifanyika kwenye maeneo mawili ya akiolojia, moja ya tangu miaka milioni 2.4 iliyopita na ya pili ya tangu miaka milioni 1.9 (Picha ya kumbukumbu) © AP
Matangazo ya kibiashara

Chimbuko la mwanadamu ni suala linalochochea utafiti mwingi wa akiolojia, ili kuelewa wapi walitokea watu wa kwanza. \

Suala hilo ni muhimu kwa fani mbalimbali, dini ikiwemo.

Kwa sasa wataalamu karibu wote wanakubaliana kwamba chimbuko la mwanadamu lilikuwa barani Afrika, lakini wanaleta ushahidi tofauti ili kupendekeza Afrika Mashariki, Kusini mwa Afrika, Afrika Magharibi au Afrika Kaskazini.

Ugunduzi huu unaweza kupoteza sifa ya Afrika Mashariki kama Chimbuko pekee la binadamu, kulingana na ripoti iliyochapishwa Alhamisi wiki hii katika gazeti maarufu la Science.

Masalia hayo yaligunduliwa katika eneo la Aïn Boucherit huko Sétif, kilomita 300 mashariki mwa Algiers, na timu ya watafiti wa kimataifa ikiwa ni pamoja na watafiti wa Algeria. Masalia hayo yanafanana na yale yanayofahamika kwa jina la Oldowan, ambayo yanapatikana hasa sasa Afrika Mashariki.

Pia waligundua mifupa kadhaa ya mifugo, ambapo kulingana na utafiti, mifupa hiyo inaonekana kuwa ni ya wanyama wa zamani kama vile mamba, tembo, kibpko au twiga.

Kwa miaka mingi, Afrika Mashariki inachukuliwa kama chimbuko la binadamu. Katika eneo hilo la Afrika mashariki kuligunduliwa masalia ya kale kuliko yote yanayojulikana hivi sasa kati ya viumbehai tangu miaka milioni 2.6 iliyopita.

Sehemu ya bonde la Ufa lijulikanalo kama bonde la Oltupai lililoko ndani ya Hifadhi ya Serengeti nchini Tanzania ndiko kulikogunduliwa masalia ya kale kuliko yote yanayojulikana hivi sasa kati ya viumbehai wanaokaribiana na binadamu.

Ushahidi wa kisayansi unaotokana na nyayo za zamadamu zilizogunduliwa eneo la Laetoli lililoko kusini kidogo mwa Oltupai umeongeza hoja kuwa Tanzania au nchi jirani ni chimbuko la binadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.